Na Daniel Mathias,
Katavi.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Robert Nyakie (40) mkazi wa Kanoge ‘A’ barabara ya tatu alikamatwa akiwa na vipande vinne vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 11.50 vyenye thamani ya Tshs 27,750,000/= ambayo ni sawa na tembo 01 aliyeuawa.
Tukio hilo lilitokea tarehe 01.03.2016 majira ya saa 14:35 huko maeneo ya kijiji cha kanoge barabara ya kwanza Kata ya kanoge Tarafa ya Ndurumo katika halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoani katavi.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa katavi ACP Rashidi Mohamedi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, siku ya tukio muda na majira tajwa jeshi la polisi kwa kushirikiana askari wa wanyama pori TANAPA walipata taarifa toka kwa raia wema kuwa katika kijiji cha kanoge kuna mtu anajihusisha na shughuli haramu za ujangiri.
ACP Mohamed alibainisha kuwa baada ya taarifa hiyo kuipata ndipo ufuatiliaji ulipofanyika kwa kuweka mtego katika nyumba ya mshukiwa na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa na vielelezo hivyo alivyokuwa amevichimbia nje karibu na ukuta wa nyumba yake.
Vilevile kaimu kamanda wa polisi huyo alifafanua kuwa jeshi la polisi mkoani hapa limeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na ujangili ambao umekuwa ni tishio katika hifadhi mbali mbali mkoa wa katavi ikiwemo kuweka doria kila sehemu hasa maeneo yanayozungukwa na hifadhi.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili mara baada ya upelelezi kukamilika.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi alitoa wito kwa wananchi kutojihusisha na shughuli haramu za ujangiri na biashara za nyara za serikali kwani ni uhalibifu wa rasilimali za taifa letu hasa kwa manufaa ya vizazi vijavyo, na kusema hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa wale wote wasiotii sheria pasipo kushurutishwa.

No comments:
Post a Comment