Monday, February 01, 2016

TFF YASEMA HAINA VITA NA ZFA


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limesema hakuna vita kati ya Shirikisho na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) bali mawasiliano yanaendelea kati ya TFF na vyombo husika kuhakikisha ZFA ambaye ni mwanachama mshiriki wa CAF anaendesha shughuli zake kwa mujibu wa taratibu.

Kanuni na taratibu za CAF ziko wazi kuhusu nani aongoze Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na anapatikana kwa utaratibu upi. Kikubwa ni kuzuia ZFA isipate madhara ya kufungiwa na Chama Cha Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).

No comments:

Post a Comment