Katika Post yake aliyoandika katika mtandao wa Instagram, Ney aliandika “Pale unaposikia eti kuna wasiopenda kuambiwa Ukweli wamezusha Eti Wimbo wa ShikaAdabuYako Basata wamefungi. Guys Wimbo haujafungiwa na Basata awajafungia Wimbo ila wale wenye Team zao kwenye mitandao wamechanwa kwenye #ShikaAdabuYako ndio wameufungia kwenye Masikio Yao sababu ya hawataki kusikia fact wame publish habari za kufungiwa. Ata ingekua kweli umefungiwa wamechelewa sanaaa coz mpaka Panya wanajua tayari #TrueBoy keshakiwashaaaaa.”
Hivi karibu Ney wa Mitego alijikuta katika wakati mgumu baada ya kutoa nyimbo hiyo ya Shika Adabu Yako, baada ya kushambuliwa na wasanii mbalimbali ambao wengi wao aliwataja katika wimbo huo. Mmoja kati ya wasanii maarufu ambaye amemshambulia Ney kwa matusi na lugha kali ni Ommy Dimpoz.
Wimbo huo umewataja kwa majina wasanii mbalimbali ukiwakashifu kwa mambo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment