Mwanamke mmoja nchini Australia, aushangaza Umati baada ya kujitokeza ghafla kwenye msiba wake mwenyewe na kudai mume wake alituma watu wamuuwe.
Noela Rukundo, ambaye alidaiwa kukaa nje ya nyumba yake akiwa ndani ya gari akiangalia watu waliofika nyumbani hapo kuomboleza, watu hao walipopungua ndipo alipomuona mume wake.
Akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Rukundo alidai kuwa siku tano kabla ya kutokea kwa tukio hilo mume wake aliyefahamika kwa jina la Balenga Kalala, alituma watu wa mauwaji kwa ajili ya kufanya kazi ya kumuuwa Rukundo.
Hata hivyo wauwaji hao walirudi kwa Kalala na kumuhakikishia kuwa walishamuuwa mwanamke huyo, ambaye ameishi nae takribani miaka 10 kwenye ndoa na kumuondolea wasiwasi na hata kumbidi kuwaongezea kiasi kikubwa cha fedha katika kuwalipa kama kwa kazi nsuri waliyofanya.
Aidha, baada ya kupungua kwa waombolezaji hao, Rukundo alishuka kwenye gari yake alimokuwa akishuhudia watu waliofika msibani hapo na baada ya mume wake kumuona alishika mikono kichwani kwa mshangao huku akidhani kuwa ni ndoto.
Rukundo alinukuu kushangazwa kwa mume wake "Ni macho yangu au naona mzimu?"alihoji mume wake huku akiwa na hofu kubwa ambapo alimjibu kuwa " Usishangae ni mimi bado naishi" alijibu Rukundo.
Rukundo alitoa taarifa polisi juu ya kutaka kufanyiwa kitendo hicho na mume wake, ambapo walifika eneo hilo na kumkamata huku Kalala akikili makosa na kukubali hukumu ya kifungo cha miaka tisa jela kutokana na sheria za nchi hiyo. Ilisema Televisheni ya Australia (ABC).
Akiieleza BBC juu ya mkasa mzima ulipoanzia, Rukundo alisema ulianza tangu mwaka uliopita wakati Rukundo na mumewe Kalala wakiwa Bujumbura kwenye msiba wa mama wa kambo na Rukundo, ambapo baada ya kumaliza mazishi Rukundo ilimbidi arudi kukaa hoteli.
Akiwa kitandani kwake katika hoteli hiyo amejipumzisha, mume wake alimtaka kutoka nje kwa ajili ya kupata hewa ambapo baada ya Rukundo kutoka nje dakika chache mume wake alitokea mbele yake na kumuoneshe bunduki kwenye bega lake la kulia.
Aliniambia "usipige kelele ukipiga kelele nakuuwa na hata kama mimi nikikamatwa lakini wewe utakuwa tayari umekufa" alimnukuu mume wake.
Hata hivyo Rukundo alifanya kama alivyo ambiwa na kuingia kwenye gari huku akiwa amefunikwa usoni bila kujua lipokuwa akipelekwa, ambapo ghafla alijikuta akitolewa kwenye kiti cha gari na kuingizwa kwenye nyumba moja.
Baada ya Rukundo kuingizwa humo ndani alisikia sauti za wanaume zikisema "We mwanamke umemfanyia nini mume wako hadi atulipe ili tukuuwe?...Kalala ametutuma tukuuwe" mmoja wa wanaume hao aliuliza.
Hata hivyo, Rukundo ambaye ana watoto wa tano huku wengine wakiwa kutoka kwa mume wake wa kwanza na watatu kwa mume wake Kalala, alidai kuwa alianzisha uhusiano na mume wake huyo baada ya kuwa mkimbizi akitokea nchini Kongo.
Alisema, alikuwa akimjua vizuri mume wake ambapo kati ya matukio ambayo aliwahi kufanya ni pamoja na kumuua mke wake na mtoto, huku akidhani kuwa vitendo hivyo hatakuja kufanyiwa yeye.
"Nilikuwa nikijua baadhi ya mambo yake, kwani hapo awali aliwahi kumuua mke wake na mtoto lakini sikudhani kama ipo siku na mimi atanifanyi ahivyo" alisema Rukundo.
Hata hivyo, alisema kuwa kati ya watu hao ambao alikuwa akiwapa fedha ili waweze kumuuwa mke wake walikuwa wakichukua fedha zake bila ya kutekeleza walichoambiwa.
" Hao watu aliokuwa akiwatuma ili waniuwe mara nyingi walikuwa wakichukua fedha zake ambapo baada ya siku mbili walikuwa wakiniachia huku yeye wakimdanganya kuwa wameshaniuwa" aliongeza Rukundo.
Hata hivyo Rukundo alisema kuwa hivi sasa anaendelea vizuri na maisha yake na kuhaidi kuwa atasimama kama mwanamke shuavu siku zote.

No comments:
Post a Comment