Friday, February 12, 2016

MAALIM SEIF ADAI MUAFAKA UMESHINDIKANA ZANZIBAR, HIVYO KUNA UMUHIMU WA KUTANUA WIGO

Katibu Mkuu wa CUF, Maaalim Seif amezungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Edward Lowassa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema, Mikocheni, Dar es Salaam. Katibu Mkuu huyo alikutana na Edward Lowassa kujadiliana mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na siasa za Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na kulinda wananchi kutokana na matukio ya wanachama wa CUF kuvamiwa na kufanyiwa fujo.

Maalim Seif alisema wamekwama kufikia muafaka katika suala la kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar, hivyo kuwepo umuhimu wa kutafuta maridhiano nje ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na Tanzania Bara, ila pia kuna kikwazo kutokana na kuwepo kwa serikali ya CCM iliyojipanga kufanya uchaguzi utakaofanyika machi 20.

“Zanzibar inaweza kukubali kama tumeshindwa kabisa katika kufikia muafaka, tunaweza kupanua wigo katika kutafuta suluhu lakini hata tukitafuta watu kutoka bara haisaidii kwa kuwa hakutakuwa na mazungumzo kwani wenzetu wameshaamua kufanya uchaguzi,labda wakubali kusitisha uchaguzi tuko tayari kwa mazungumzo na kufikia muafaka,”alisema Maalim Seif







No comments:

Post a Comment