Kwa miaka mitano sasa, pamekuwa na mshindi mmoja tu,
hatimaye Sepp Blatter, mtu aliyefungiwa na kusemwa vibaya amefikia mwisho na
nafasi yake kuchukuliwa na Gianni Infantino, Rais mpya wa shirikisho la soka
ulimwenguni FIFA.
Ushindi wa Infentino unahesabika kama moja ya mafanikio
makubwa katika siasa za soka ulimwenguni. Miezi mitano iliyopita wala
hakufikiria kugombea nafasi hiyo ya juu, huku bosi wake Michel Platini ndiye
aliyefikiriwa kumrithi mtangulizi wake, Blatter.
Lakini kutokana na kashfa iliyoibuliwa na maofisa kutoka
Uswiss kuhusiana na malipo ya kiasi cha shilingi bilioni 39.8 (£1.3m), mipango
yote ikaharibika na kubadilisha kila kitu. Infentino awali aliingia kama
mgombea ili kutia joto kiti cha Platini ikitokea akaponea uchunguzi wa FIFA.
Kwa maana kwamba Platini angeshinda uchunguzi huo basi ni
wazi Infetino asingegombea nafasi hiyo. Hata hivyo watu wengi walihisi uwepo wa
Infentino katika kinyang’anyiro cha Urais wa FIFA ulikuwa ni mtego wa
kuhakikisha hakuna mgombea kutoka bara la Ulaya atakayepita ili kumhakikishia
Sheikh Salman wa Bahrain ushindi.
Lakini kampeni zilivyozidi kukolea, Infentino alionesha wazi
kuwa yuko katika mbio hizo kushinda. Akipata ufadhili wa dola za Marekani
500,000, alianza safari kwenda nchi mbalimbali, huku wapinzani wake wakiendelea
kupigia debe na kukutana na swali la jinsi Bahrain inavyopinga uwepo wa
demokrasia nchini humo, ndipo alipoamua kufanya kweli.
Hatimaye ikalipa, wakati wakijaribu kushawishi wapiga kura
waliomlinda Blatter na waliomtaka Salman, mikakati ya ikavurugika na kuongeza
shinikizo dakika chache zilizobaki, huku kikwazo pekee kikionekana kuwa ni Infentino
na kundi lake la UEFA.
Ushindi wa Infentino utaondoa mawazo ya zamani kuwa ulikuwa
ni mpango wa Blatter kumuachia kiti Platini na uchaguzi huo huwa unapangwa
kwani yeye amechaguliwa kihalali.
Ushindi huo ni mwanzo tu. Infentino ambaye ni mzaliwa kutoka
mji ulioko umbali wa maili 10 toka kwa nyumbani kwa Sepp Blatter, atategemewa
kuonesha kuwa yeye ni kiongozi tofauti na tabia zake hazifanani na waliomtangulia.
Yeye anaijua soka, na ameshakutana na kashikashi na kashfa
za UEFA kuhusiana na upangaji matokeo. Lakini pia anaonekana ni bora zaidi
kutokana na kashfa zilizoikumba FIFA. Hata hivyo haitokuwa kazi rahisi kwake.
Shirika hilo bado liko kwenye mikono ya sheria nchini Marekani na Mwendesha
Mashtaka nchini Uswiss.
Maofisa wamekuwa wakitangaza mipango na madili mbalimbali
kuhusiana na mipango ya kombe la dunia kwa miaka mitano sasa, jambo ambalo
linaliweka shirika hilo katika uchunguzi.
Infantino ataonekana wa maana zaidi ya Salman kama atatoa
ushrikiano kwa wanasheria wa Zurich ambao nao wanashirikiana na FBI wa Marekani,
na iwapo atafanya hivyo, basi ulimwngu utarudisha imani kwenye soka na FIFA na
yeye.
No comments:
Post a Comment