Friday, February 19, 2016

EXCLUSIVE: JAYDEE KUZINDUA NGOMA MPYA KWA UBUNIFU MKUMBWA...FUATILIA

Na Mwandishi Wetu

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura ‘Jaydee’ amejipanga na anakuja ngoma mpya itakayojulikana kama ‘Naamka Tena’ inayotegemea kutoka tarehe 20 March, 2016. Katika maandalizi ya release hiyo, Jaydee ametumia ubunifu wa aina yake kwa kuwashirikisha watu maarufu nchini kupromot wimbo huo mpya.

Akizungunza na blog ya immamatukio, msaidizi wa msanii wa Jaydee, Bw. Wancy Nells, alisema Safari hii mtaona ubunifu ulivyochukua nafasi yake katika tasnia ya muziki, tumewashirikisha watu maarufu katika promotions kabla ya kufikia siku ya kutoa ngoma hiyo.”

Ikiwa leo ni siku ya kwanza ya kampeni hiyo, video clip ya kwanza kutoka ni inamuonesha mchora katuni maarufu nchini, Masoud Kipanya akianza kwa kuonesha Kipanya akitambulisha siku ya 30(angalia video juu) kabla ya kutoka ‘Naamka Tena’.


Lady JayDee amesha zoa tuzo zaidi ya 30 ndani na nje ya nchi ambazo ni pamoja na Channel O, BBC, Afrimma, Kisima, KTMA, na Bingwa, na kujizolea umaarufu nchini na kimataifa.

“Tunafurahi na kuridhishwa na maadalizi kabla ya tarehe 20. Kati ya watu maarufu 30 tuliowashirikisha, wapo Mawaziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Wakuu wa Wilaya.”

Sura nyingine zinazotarajiwa kuonekana katika siku hizo 30 kuanzia leo ni pamoja na waigizaji maarufu nchini, Wanamitindo maarufu na wasanii wengine.­­


No comments:

Post a Comment