Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Balozi Simba Yahya (katikati) pamoja na ujumbe wake, wakiingia katika lango kuu
la kuingilia abiria wakati alipotembelea eneo kilipozama kivuko cha MV
Kilombero II na kushuhudia shughuli za uokoaji wa magari, utafutaji miili ya watu
na uokoaji wa kivuko hicho ukiendelea. Balozi Simba alifanya ziara ya kikazi mkoani
Morogoro kwa kutembelea miradi ya maendeleo ya Jeshi la Magereza mkoani humo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Balozi Simba Yahya (kulia), akisalimiana na Askari wa Kikosi cha Wanamaji wa Uokoaji
wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao wanashiriki katika shughuli za uokoaji miili
ya watu waliozama baada ya kivuko cha MV Kilombero II kuzama Januari 27.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Balozi Simba Yahya akiongozana na ujumbe wake kuelekea eneo la tukio ambapo
kivuko cha MV Kilombero II kilizama wiki iliyopita. Kulia ni Kamishna wa Sheria
na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa. Katikati ni Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Morogoro, SACP Dkt.
Kato Lugainunura.
Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero, Yahya Naniya (kulia), akitoa
maelezo juu ya shughuli za uokoaji zinavyoendelea kwa Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wa tatu kushoto) na
ujumbe aliofuatana nao mara baada ya kufika eneo kilipozama kivuko cha MV
Kilombero II wiki iliyopita. Naibu Katibu Mkuu alikuwa mkoani Morogoro mwishoni
mwa wiki kwa ziara ya kikazi.
Wasamaria wema waliojitolea kushiriki zoezi la uokoaji
katika ajali ya kivuko cha MV Kilombero II kilichotokea wiki iliyopita mkoani
Morogoro, wakimuelekeza dereva wa gari la kunyanyua vitu vizito (halipo
pichani), wakati wa uokoaji wa moja ya magari yaliyozama wakati wa ajali hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) na ujumbe aliofuatana nao wakiangalia shughuli za uokoaji zinavyoendelea mara baada ya kivuko cha MV Kilombero kuzama huku baadhi ya vitu vikiokolewa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi
Simba Yahya, akiondoka eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero mara baada ya
kushuhudia shughuli za uokoaji zikiendelea vizuri. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
No comments:
Post a Comment