Monday, January 18, 2016

MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)MH. SULEIMAN SAID AFARIKI DUNIA, KUZIKWA LEO

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) KULIA PICHANI, Mhandisi Suleiman Said amefariki dunia mapema leo asubuhi akiwa katika mazoezi ya kuogelea,taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Suleiman alikimbizwa hospitali ya Agakhan kwa matibabu na baadae ikaelezwa kuwa amekwishafariki na kuwa mazishi yanatarajiwa kufanyika leo. Marehemu alipata kuwa Katibu mkuu wa Simba.

Taarifa zaidi zinasema Marehemu Mr Sukeiman aliamka asubuhi akamwambia mke wake hajiskii vizuri, lakini alienda baharini kuogelea kama kawaida yake. 

Walikuwa wawili na mwenzie, wakaenda mbali sana wakati wa kirudi aliishiwa nguvu, alijitahidi akafika nchi kavu akiwa hoi kabisa amekunywa maji wengi na akawa anatokwa na mapovu mdomoni. Alifariki njiani akipelekwa hospitali. 

Msiba upo upanga nyuma ya jeshi (Ngome) saa hii maiti imefuatwa wanakuja kuaga hapa nyumbani, mwili utarudi msikitini saa tisa kisha kuzika makaburi ya Kisutu nyuma ya chuo cha CBE. Apumzike kwa Amani.


No comments:

Post a Comment