Wednesday, November 18, 2015

HAPA KAZI TU: KAMA ULINUNUA KIWANDA NA MASHIRIKA YA SERIKALI HII INAKUHUSU

Na Mwandishi Wetu
Serikali imetoa tamko kuwa baada ya siku 30 kuanzia sasa itarejesha mashamba na viwanda vyote vilivyobinafsishwa na wamiliki wake kukiuka masharti na kushindwa kuviendeleza.

Kauli hiyo imetolewa na ofisi ya msajili wa Hazina na kusainiwa na Lawrence Mafuru ambayo ndiyo imepewa majukumu ya kusimamia mali za serikali “ninawaagiza wawekezaji wote walionunua viwanda na mashamba yaliyokuwa yakimilikiwa na serikali kuwa wawakilishe taarifa zao za utekelezaji wa mkataba wa mauzo kwenye ofisi ya hazina”taarifa hiyo ilieleza.

Ofisi ya hazina imepewa mamlaka hayo kupitia tamko la serikali namba 203 na kuchapishwa juni 27,2014 pia kupitia sheria yake ya Treasury Registrar(power and function)Act,sura ya 370 na kurekebishwa mwaka 2010 imempa mamlaka ofisi ya Hazina kusimamia mashamba,viwanda na mali nyingine za serikali .

Taarifa hiyo inasema kuwa ofisi ya msajili wa Hazina kwa sasa inarejea mikataba yote ya mauzo ya viwanda na mashamba iliyoingiwa kupitia mpango wa ubinafsishaji na lueleza kuwa iwapo mikataba haijafuatwa hatua zitachukuliwa kwa wahusika. 

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa wawekezaji wamekiuka masharti ya mikataba waliyokubaliana wakati wanachukua mashamba na viwanda hivyo,aidha taarifa hiyo ilibainisha mambo yaliyokiukwa kuwa ni pamoja na kutoendelezwa kwa viwanda na mashamba kwa mujibun wa mikataba.

Pia mambo mengine yaliyoelezwa katika taarifa hiyo ni kushindwa kutekelezwa mpango wa uwekezaji na na baadhi ya wanunuzi wa viwanda hivyo kuuza mashine walizozikuta bila kurudishia mashine mbadala kinyume na makubaliana yaliyoandikwa katika mikataba.

Mbali na hayo pia taarifa hiyo ilibainisha mambo mengine kuwa ni kutokamilisha kwa malipo ya ununuzi wa viwanda na mashamba na mwisho wale waliobadilisha matumizi ya ya viwanda na mashamba bila idhini.

Taarifa hiyo inawataka wamiliki wote waliobinafsishiwa mashamba na viwanda kupeleka taarifa zao ndani ya siku 30 kinyume na hapo hatua stahiki zitachukuliwa ikiwemo kurejeshwa mashamba na viwanda hivyo mikononi mwa serikali.

Ikumbukwa kuwa moja ya ya mambo yaliyochukua nafasi wakati wa kampeni ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kuhakikisha kuwa tunafufua viwanda vilivyokufa na kutoa nafasi zaidi kujenga vingine ili kutuwezesha kufikia lengo la nchi zenye uchumi wa kati.

http://www.tro.go.tz//docstation/com_content.article/119/press_release___kurejeshwa_kwa_viwanda_vilivyokiuka_masharti_ya_mikataba.pdf


No comments:

Post a Comment