Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri na Wakurugenzi wa Hospitali za Rufaa, ulioanza leo Sept 8, 2015 na Maadhimisho ya Miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye Hoteli ya Blue Peal Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Dkt.Bilal, akimkabidhi Tuzo Naibu Waziri wa Afya, Stephen Kebwe, kwa mchango mkubwa wa kuiongoza Wizara hiyo.
Msanii Mrisho Mpoto na wasanii wa kundi lake la Mjomba Band,wakiigiza kutoa ujumbe katika hafla huyo.
Makamu wa Raus wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Bilali akimkabidhi cheti Prof.Janabi kutoka kitengo cha moyo Mihimbili kwa kutambua mchango wake kama mmoja ya walioshiriki jitihada ya kudhibiti Ebola Afrika Mashariki.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akihutubia kufungua rasmi Mkutano huo.
Hapa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na washiriki wa mkutano huo mara baada ya kuufungua.PICHA NA OMR.
MKAMU wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal ameipongeza Wizara ya afya na ustawi wa jamii ,katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kifua kikuu pamoja na kupambana na tatizo la hivi karibuni la mlipuko wa ugonjwa wa kipindipindu jijini Dar es salaam.
Ameyasema leo katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa waganga wakuu wa Mkoa ,halmashauri na wakurugenzi wa hospital za rufaa katika maadhimisho ya miaka 40 ya mpango wa taifa wa chanjo.
Amesema kuwa Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika zilizopiga hatua katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake hususani zinazolenga kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kwa kutekeleza hatua mbalimbali pamoja na kuongeza kiwango cha chanjo.
''imethibitika kuwa chanjo ni mkakati muafaka katika kutokomeza magonjwa na kupunguza vifo vya watoto hivyo kupunguza gharama kubwa ambazo familia zetu na taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu maradhi yanayotokana na magonjwa yanayozuilika'' anasema Dkt Bilal
Pia amesisitiza jitihada zaidi zinatakiwa ili kuongeza na kuboresha huduma za afya katika kuokoa maisha ya watoto hususani wachanga.
Amesema katika kuboresha huduma za afya Nchini Serikali imepata mafanikio makubwa ambapo vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka 3,619 mwaka 2005/06 hadi kufikia 7,247 mwaka 2014/15 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya 100% ambapo ongezeko la vituo limechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa huduma za afya zinazotolewa karibu na wananchi hususani vijijini.
Aidha ameipongeza Wizara kwa kuanzisha huduma ambazo awali zilikuwa hazipatikani hapa nchini kama upasuaji wa moyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambazo kwa kiasi kikubwa zimeiwezesha Serikali kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa nje ya nchi.
Ufunguzi huo pia umeambatana na ugawaji wa zawadi na vyeti kwa Mawaziri wa Afya wastaafu,Makamu wastaafu ,Makatibu wakuu,Waganga Wakuu wa Serikali pamoja na mikoa iliofanya vizuri katika elimu ya chanjo mwaka 2014 mikoa hiyo ni pamoja na Pwani ,Mwanza na Mbeya pamoja na wilaya ya Rufiji,Mbalali,Kibondo,Musoma na Rombo.
Hata hivyo amewataka wafanyakazi kupitia mpango wa utekelezaji wa matokeo makubwa sasa kila mmoja kujitathimini utendaji wake wa kazi na kubadilika kutokana na mustakabali wa Afya za Wananchi ipo mikononi mwao.
No comments:
Post a Comment