Mgombea urais kupitia umoja wa Katiba ya Wananachi (UKAWA) Edward Lowassa l(Pichani kushoto) leo amezua gumzo baada ya kuonekana akiwa ndani ya dadala katika maeneo ya Gongo la Mboto jijini Dar es saalam.
Inadaiwa kuwa Mgombea urais huyo aliamua kupanda daladala katika root ya Gongo la Mboto Chanika ili kujionea kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo hayo hali iliyozua tafrani kwa wananchi kutaka kumuona kufuatia tukio hilo kuwa la kushitukiza.
Katika hatua nyingine vyama vnavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA vimeshindwa kuznidua kampeni zake jijini Dar es salaam jumamosi iliyopita kufuatia kuzuiwa na serikali kuutumia uwanja wa Taifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia alisema kuwa umoja huo unatafakari ni wapi wakafanyie zoezi la kuzindua kampeni hizo kwa madai kuwa wanataka sehemu yenye usalama na itakayobebaba watu wengi zaidi kwa kuwa maeneo mengi ya wazi yalishauzwa kwa watua binafsi.
No comments:
Post a Comment