Monday, June 09, 2014

RONALDO: HII NDIO SIRI YA MAFANIKIO YANGU, NAMSHUKURU SANA RAFIKI YANGU

“Napenda sana kumshukuru rafiki yangu wa zamani Albert Fantrau kwa mafanikio yangu. Tulicheza pamoja tulipokuwa watoto.” Hayo ni maneno ya mchezaji maarufu mwenye uraia wa Spain, Cristiano Ronaldo alipokuwa akiongea na kueleza jinsi ambavyo ni muhimu kukumbuka watu waliochangia mafanikio yake.

Anasema wakati watu kutoka Sporting Lisbon Academi walipofika kuchagua wanafunzi katika mchezo wa soka, waliwaahidi kuwa atakayefunga magoli mengi atasomeshwa katika chuo chao.

“tulishinda bao 3 – 0” anaeleza Cristiano, kwamba yeye alifunga goli moja la kwanza na kisha rafiki yake huyo akafunga goli gumu sana, isipokuwa goli la tatu lilimfurahisha kila aliyeshuhudia mchezo ule.
Anasema Albert alikuwa uso kwa uso na kipa , wakati yeye yuko pembeni wanafuatana, akamzunguka kipa na alichotakiwa kufanya ni kupiga tu mpira golini kwani lilikuwa wazi tu. “Lakini, akanipasia na mimi nikafunga goli.” Aliendelea Ronaldo. Kutokana na goli hilo Cristiano alipata skolaship akaenda kusoma katika chuo cha Sporting Lisbon Academy kama ahadi ilivyotolewa. 

Lakini baada ya mchezo kwisha Cristiano alimfuata Albert na kumuuliza kwanini alifanya vile? Albert alimjibu kuwa “we unacheza vizuri zaidi yangu” Ronaldo alienedelea na shule na kukua zaidi katika soka na ndio Cristiano tunayemsikia sasa katika ulimwengu wa mpira. 

Miaka ilizidi kupita na hatimaye siku moja mwandishi alikwenda nyumbani kwa Albert kumuuliza kama hiyo story aliyoieleza Cristiano ina ukweli wowote. Albert alidhibitisha kuwa ni kweli.

Albert anasema kuwa hata taaluma yake ya soka iliishia palepale uwanjani katika mchezo ule walioshinda magoli 3 – 0, lakini kama haitoshi sasa hivi hana kazi. Lakini mwandishi hakuishia hapo na kumuuliza kuwa anapata wapi pesa zote hizo alizonazo kwa maana anaishi kifahari sana.

Ana magari ya gharama na nyumba kubwa na kwamba anaoneakana ni tajiri analisha familia yake, yote haya yanatokea wapi?

Albert alijibu kuwa “vinatoka kwa Cristiano”


No comments:

Post a Comment