Katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Kombe la Dunia 2014,
Brazil imeibuka na ushindi wa magoli 3 - 1 dhidi ya Croatia, katika mechi
iliyochezwa leo ambapo mchezaji bora katika mechi hiyo bila mashaka aliibuka
kuwa Neymah
Goli la kwanza kufungwa katika kipindi cha kwanza lilikuwa
ni la Croatia ambapo, beki wa Brazil, Marcelo alijifunga wakati akijaribu
kuokoa ikiwa ni dakika ya 12 baada ya
mpira kuanza.
Hata hivyo furaha ya goli hilo ilizimwa baada ya
mshambuliaji wa Brazil Neymah kupata goli la kwanza ikiwa ni dakika ya 29,
baada ya kupiga shuti refu lililogonga mwamba na kuingia langoni bila ubishi.Mpaka
kipindi cha kwanza kinakwisha timu hizo zilikuwa sare ya 1 -1.
Kipindi cha pili kilianza kwa mpira wa wastani ambapo katika
dakika ya 71.50 mshambuliaji wa Brazil, Danny Alves alipokuwa anaelekea kufunga
alichezewa madhambi kwakushikwa na Roll na kusababisha penalty ambayo ilipigwa
na Neymah na kuipa Brazi goli la pili.
Katika dakika ya 91 ikiwa ni mda mchache baada ya Neymah
kutoka, Oscar aliipatia Brazil goli la 3 baada ya kuachia shuti kali huku akiwa
katika mwendo mkali. Kipa alijitahidi lakini jitihada zake hazikuzaa matunda na
mpaka mpira unaisha Brazil 3 Croatia 1.
No comments:
Post a Comment