Vurugu kubwa zimetokea mkoani Mbeya baina ya Jeshi la Polisi na waendesha bodaboda(pikipiki) baada ya jeshi la polisi kutaka kuzima jaribio la kutaka kuvunja nyumba.
Boda boda hao walifunga barabara na kuzua taflani baina yao na jeshi la Polisi baada ya Jeshi hilo kuingilia kati kumuokoa Mke wa dereva wa pikipiki baada ya madereva hao kuvamia nyumba yake maeneo ya Forest wakitaka kubomoa wakimtuhumu kuhusika na kifo cha mumewe.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa nne asubuhi baada ya waendesha bodaboda kutaka kumdhuru mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua dereva mwenzao ndipo jeshi la polisi lilipoingilia kati hivyo kusababisha vurugu kubwa baina ya madereva hao na jeshi la polisi.
Hata hivyo madereva wa pikipiki zaidi ya 20 walilivamia gari la Polisi na kuvunja kioo cha mbele hali iliyopelekea dereva wa gari hilo kulikimbiza hadi kituo cha Polisi cha Kati ili kuomba msaada kwa askari wenzie waliojitokeza wakiwa na silaha za moto na kuwatawanya kabla ya kufunga barabara na kuanzisha vurugu. (via Mwitiko Blog)
No comments:
Post a Comment