Monday, March 17, 2014

MAKUBWA: AJIPIGILIA MISUMARI KICHWANI, AISHI KIMAAJABU (ONA PICHA)


*AZUIA TAARIFA ZISIFIKE POLISI


Mtu ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja ambaye ni Mchina, anaishi kwa maajabu baada ya kujipigilia misumari 3 yenye urefu wa cm 10 kwenye kichwa chake.

Kama picha inavyoonesha pamoja na picha ya xray, misumari hiyo imepigiliwa kwenye fuvu la kichwa na kuingia kwenye ubongo, amini usiamini. Hata hvyo mtu huyo alifanyiwa upasuaji na kurudia katika hali yake ya kawaida miezi mitatu baadaye.

Pamoja na kwamba mtu huyo alisistiza kuwa alijifanyia tukio hilo mwenyewe, madaktari wanaamini kuwa mtu huyo atakuwa amepigiliwa hiyo misumari na mtu mwingine kutokana na nguvu iliyotumika kushindilia misumari hiyo.

Kwa sababu hiyo hakuna mtu yoyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Zaidi ya hilo bwana huyo aliomba polisi wasipewe taarifa.

No comments:

Post a Comment