Thursday, March 13, 2014

KUNDI JIPYA LAZUA VURUGU ZANZIBAR, LAHARIBU MALI ZA SERIKALI

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa kikundi cha vijana Zanzibar kinachojiita UbayaUbaya kimeanza kuleta vurugu na kuanza kupiga mawe magari ya serikali huku wakijerui wafanyakazi wa serikali.

Akidhibitisha tarifa hizo kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mjini Magharib, RPC Mukadam, amesema anazo taarifa hizo na anfuatilia tukio hilo.

"Ni kweli nimepokea taarifa hizo na vijana wamekwenda kufuatilia ili kujua ni magari mangapi na ya idara zipi za serikali yaliyoshambuliwa" alisema Mukadam.

Aidha RPC Mukadam ameeleza kuwa chanzo cha vurugu hizo ni operesheni ya kiusalama iliyokuwa ikiendeshwa ndio imesababisha vijana hao kuanzisha fujo hizo. Alisema "imekuwa kawaida yao kila mara kukiwa na operesheni kama hizo wao huanza kushambulia mali za serikali"

SOMA ZAIDI . . .

Kati ya walioshambuliwa masaa machache yaliyopita ni pamoja na gari la Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Mh. Khamis Musa lenye namba za usajili SMZ249A ambalo lilipinduliwa katikati ya barabara, inadaiwa katika gari hilo Katibu Mkuu huyo hakuwepo. dereva wa gari hilo inadaiwa anaendelea vizuri.

Kamanda Mukadam, alidhibitisha kuwa sio Jumuiya ya Uamsho kama watu wengi wanavyozusha, bali ni kikundi cha vijana wanaojiita Ubaya Ubaya.


No comments:

Post a Comment