Wednesday, March 19, 2014

CHELSEA YASHINDA 3 - 1 DHIDI YA GALATA

Chelsea ndiyo timu ya pekee ya Uingereza iliyojihakikishia nafasi ya kushiriki mechi za robo fainali za ligi ya mabingwa barani uropa baada ya kuinyamazisha Galatarasay ya Uturuki mabao 2-0 katika mechi iliyokuwa ikitazamiwa na wengi katika uwanja wa Stamford Bridge.

Matokeo hayo yanaipa Chelsea ushindi wa jumla ya mabao 3-1. Hatua ya kocha Jose Mourinho kumpumzisha mshambulizi wake Fernando Torres na badala yake kumchezesha nyota wa Cameroon Samuel Eto'o ilizaa matunda punde baada ya kipenga cha kwanza.

Etoo ambaye majuzi alikejeliwa kutokana na umri wake mkubwa alimnyamazisha Mourinho kwa kufuma bao la kwanza kunako dakika ya nne na kufufua matumaini ya mashabiki wa Chelsea na haswa Uingereza katika uwanja wa Stamford Bridge.

Wawakilishi wengine wa Uingereza Manchester city na Arsenal tayari wamebanduliwa nje ya mashindano hayo kwa hivyo matumaini ya waingereza ilikuwa ni kwa Blues inusuru hadhi yao.

Chelsea haikuzembea iliendeleza gonga gonga hadi dakika tatu kabla ya kipenga cha mwisho wa kipindi cha kwanza,,, mkwaju wa John Terry ulipotemwa na kipa wa Galatasaray Fernando Musiera na kisha Garry Cahili akacheka na wavu na Kuihakikishia Chelsea fursa ya kusonga mbele.

Timu hizo zilikuwa zimetoka sare ya moja kwa moja katika mkondo wa kwanza uliochezwa Uturuki. Licha ya sifa kedekede mshambulizi wa Galatasaray Didier Drogba alishindwa kunawiri StamfordBridge ila kushuhudia timu yake ya zamani ikifuzu kwa awamu ya robo fainali ya kombe la mabingwa

Drogba ambaye alikuwa amelimbikiziwa sifa na Jose Mourinho kuwa ni moja kati ya washambulizi bora zaidi duniani hakupata fursa ya kufanya mashambulizi na badala yake alionyesha kadi ya njano na refarii Felix Brych kwa kucheza visivyo .

Licha ya tajriba kubwa Kocha wa Galatasaray Roberto Mancini hajamshinda mwenzake wa Chelsea Jose Mourinho in katika mechi sita walizokutana. Aidha timu hiyo kutoka Uturuki imeshindwa na timu za kutoka Uingereza katika mechi nane walizocheza za ligi ya mabingwa barani Uropa.

Le blues watajiunga na Vinara wa ligi kuu ya Uhispania Real Madrid ambao walifuzu kwa hatua ijayo baada ya kuitokomeza Shalke 04 ya Ujerumani mabao 3-1 na hivyo jumla ya 9-2 katika mechi ya pili iliyochezwa leo huko Bernabu. (bbc)

No comments:

Post a Comment