Tuesday, February 11, 2014

WAUA MTOTO KWA ADHABU YA KUMYWESHA JUIS YA MATUNDA

Wanandoa wameshtakiwa kwa kosa la kumuua mtoto wa miaka mitano baada ya kumlazimisha kunywa lita mbili za juisi ya zabibu pamoja na maji ikiwa ni adhabu yake.

Alex Linboom alikimbizwa na baba yake Randall Vaughn(pichani mwisho kulia)  hospitali januari 1, 2012 pamoja na mkewe, Mary baada ya mtoto huyo kubadilika rangi na kuwa wa bluu, alieleza Sharif wa kaunti ya Hawkins, huko Tennessee nchini Marekani

Mtoto huyo alikuwatwa na matatizo makubwa ya ubongo yaliyosababishwa na wingi wa vinywaji hivyo. Vinywaji hiyvo vilimsababisha ubongo wake kuvimba na kusababisha kifo chake.

Baada ya uchunguzi wa miaka miwili, wapelelezi waligundua kuwa msichana huyo aliuawa, na wanandoa hao wamehukumiwa.

“Tuliochogundua ilikuwa ni suala la muda tu baada ya mtoto huyo kuanza kuonesha dalili za kifo, mtoto huyo alianza kupiga kelele kutokana na maumivu makali, akapooza na kuzimia” alisema mwendesha mashtaka Berkeley Bell.

“Mtoto huyo alikuwa amepewa adhabu ya kulazimishwa kunya juisi ya zabibu, na kunywa maji mengi kiasi kwamba mwili wake ukatengeneza sumu iliyotokana na maji” aliongeza Bell.

Randall Vaughn, 41, na mkewe mwenye umri wa miaka 58, wanazuiliwa kusubiria dhamana.





No comments:

Post a Comment