Sunday, February 02, 2014

MASHOGA KUWAKILISHWA BUNGENI, WATATEUA MGOMBEA WAO


Shughuli ya kupiga kura Afrika Kusini
Chama kipya kinachowatetea wapenzi wa jinsia moja kitasimamisha wagombea nchini Afrika Kusini mwaka huu.

Msemaji wa chama hicho cha Equal Rights, Michael Herbst amesema kuwa chama hicho kiliundwa ili kuwalinda wanawake wanaobakwa na wanaume wanaodai kuwa wanataka kuwaondoa katika usagaji.

Ameongezea kuwa watoto ambao wanaonewa kwa kuwa wanadaiwa kuwa wapenzi wa jinsia moja wanahitaji sauti ya kuwasaidia.

Katiba ya Afrika Kusini inapinga ubaguzi wowote kutokana na maswala ya jinsia na kwamba ndoa za watu wa jinsia moja zinaruhusiwa.

Lakini waandishi wanasema kuwa mapenzi ya jinsia moja ni mwiko katika maeneo mengi ya mashambani pamoja na yale ya mijini.(BBC)


No comments:

Post a Comment