Katika tukio hilo Dar es Salaam jana gazeti hili ilishuhudia mara baada ya doria ya kawaida kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya na kikosi cha doria wanamaji wakifanya upekuzi katika meli hiyo na kubaini kuwa kuna chumba kilichochimbwa kwenda chini ya jahazi ambapo kimesindikwa shehena ya dawa hizo.
Akizungumza baada ya kupakua shehena hiyo ya madawa Kamishina Polisi Msaidizi na kamanda wa kikosi cha wanamaji Mboje Kanga alisema kikosi chake kwa kushirikiana na kikosi cha madawa walibaini jahazi hilo linalotoka Iran juzi usiku saa sita hivyo kutilia shaka kutokana na uchakavu wake hivyo kuhitaji kulipekua.
Alisema jahazi hilo lililokuwa na watu 12 ambapo Raia wa Pakistani ni wanne na raia wa Iran ni nane lilifanyiwa upekuzi wa kutosha kwa kusaidiana na wakufunzi wa polisi kutoka Marekani ambao wamekuja kutoa mafunzo kwa polisi wanamaji wa Tanzania jinsi ya kunasa madawa ya kulevya hatua ambayo iliwezesha kubaini kuwa katika jahazi hilo kuna chumba kilichombwa na kufukiwa shehena hiyo.
Alisema thamani halisi ya madawa hayo haijajulikana wala mtandao uliokuwa ukitarajiwa kupokea mzigo huo nchini kwani watuhumiwa hao wamegoma kuzungumza lugha yeyote zaidi ya kipakistani na kiarabu hivyo upelelezi zaidi unaendelea.
Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha kudhibiti madawa ya kulevya nchini Godfrey Nzoa alisema madawa hayo yanayodhaniwa kuwa ni Heron yaliyokamatwa ni kiashiria cha muendelezo wa vitendo vya uhalifu katika biashara harama ya madawa ya kulevya hivyo kikosi chake kimejipanga ipasavyo kukabiliana na uhalifu huo.
Alisema kwa kushirikiana na watu wa Intepool wamekuwa na mafanikio makubwa kupata wahalifu wa matukio hayo kutoka nchi mbalimbali ambapo katika tukio hilo wamebaini jahazi lililobeba mzigo huo linaitwa Aldanial ambalo limetoka nchini Iran na mmiliki wake ni Raisee wanchi hiyo.
Aidha watuhumiwa wa awali katika tukio hilo ni pamoja na Nahodha wa Jahazi hilo Bw. ,Ayoub Hot (50) raia wa Iran, Abdulsamad Badreuse (47) raia wa Iran,Muhamad Hasan (30) Raia wa Pakistani,Hazra Azat (60) Iran,Nahim Musa(25) Iran,Khalid Ali (35) Iran,Abdul Nabii (30) Pakistan,Rahim Baksh(30) Pakistan,Kher Mohamed (75) Iran,Said Mohamed (34) Iran,Murad (38) Iran na fahiz Mohamed (34) Pakistan.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi Chaz Tizebe akishuhudi tukio hilo alisema ni wakati muafaka mataifa yanayodhani kuwa Tanzania ni uchochoro wa biashara haramu ya dawa za kulevya kufuta dhana hizo kwani hatua zaidi zitachukuliwa kukabiliana na wote wanaohusika katika matukio hayo ili kujenga heshima ya nchi.
Alisema mbali na kukamata watuhumiwa hao wataendelea kuwatangaza na vyombo vya sheria kuchukua hatua zaidi na hakuna atakayeachwa katika sakata hilo.
“Tanzania si uchochoro wa biashara hii harama na tutahakikisha tunawachukulia hatua kwelikweli hasa hawa jamaa,na kama ningekuwa ni mimi natoa hukumu ningewakata vichwa hawa kwani wao wanaua maelfu ya vijana wetu ni watu hatari sana mzigo mkubwa kama huu ni vijana wangapi nguvu kazi ya Taifa hili wangekuwa mazezeta,matahira au hata kubebeshwa kupeleka nchi nyingine inasikitisha sana, maoni kwa Wabunge wenzangu ni muhimu kuelewa kuwa hili ni tatizo la nchi nzima adhabu haitoshi wakati umefika kuamua kutunga sheria kali ambayo itawafanya watu hawa kujuta na kutokurudia kuchezea nchii hii.”alisema
No comments:
Post a Comment