Wednesday, January 01, 2014

WAZIRI WA FEDHA DK.WILLIAM MGIMWA AFARIKI DUNIA

Taarifa za hivi punde zinasema Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa amefariki dunia.

Waziri huyo katika serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete amefariki dunia hii leo baada ya kuugua na kulazwa nchini Afrika Kusini.

Mgimwa aliyezaliowa January 20, 1950 na kuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) alilazwa katika Hospitali ya Binafsi ya Milpark ya nchini Afrika Kusini.

Dk. Mgimwa alikuwa mkufunzi katika Chuo cha Benki mkoani Mwanza, kabla ya kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Mkoa wa Iringa, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.



No comments:

Post a Comment