Sharon alizaliwa katika eneo la Palestina mwaka 1928. Alipigana katika vita kati ya waarabu na wapalestina kati ya mwaka 1948-49 na kuongoza majeshi ya Israel mapema miaka ya hamsini
Mwaka 1971, Sharon aliamuru kuharibiwa kwa nyumba 2,000 za wapalestina katika juhudi zake za kukabiliana na wapiganaji wa kipalestina waliokuwa wanapigania uhuru wa Palestina
Mwaka 1973, Sharon alihudumu katika jeshi wakati wa vita vya Mashariki ya Kati. Kama waziri wa kilimo chini ya utawala wa Menachem Begin, aliunga mkono sera ya kujenga makazi ya walowezi katika eneo la Palestina
Kama waziri wa ulinzi Sharon alioongoza uvamizi dhidi ya Lebanon mwaka 1982. Alifanya hivyo ili kuwezesha wanajeshi wakristo wa Phalangist kuingia katika kambi za Sabra na Shatila kuwasaka wapiganaji wa PLA.
Maelfu ya watu walifariki katika vita hivyo, na kupelekea wapalestina kumuita Sharon muuaji. Waisraeli, 400,000 waliandamana kupinga matamshi hayo. Sharon aliungwa mkono na mkewe wa pili Lili na wanawe Omri na Gilad. Mkewe wa kwanza Margalit alifariki katika ajali ya barabarani, mwaka 1962. Mwanawe Margalit alifariki mwaka 1967 katika tukio la ufyatulianaji risasi. Naye Lili alifariki mwaka 2000
Sharon alijiondoa katika siasa na wala hakuonekana sana hadharani akitoa matamshi ya kisiasa baada ya kustaafu. Lakini mapema miaka ya 1990, nyota yake ilianza tena kung'aa na mwaka 1999 alichaguliwa kama kiongozi wa chama cha Likud.
Sharon alianza kuwaondoa walowezi kutoka katika ukanda wa Gaza na maeneo machache ya Ukingo wa magharibi mwaka 2005. Kitendo chake hicho kiliwaghadhabisha baadhi ya wafuasi wake na kumlazimisha kudhibiti usalama zaidi
Mnamo mwezi Septemba mwaka 2000, huku hali ya taharuki ikishuhudiwa, ziara ya Sharon katika Hekallu la Mount/Dome eneo takatifu kwa wakristo na waisilamu, ilizua utata na kuchochea harakati za waplestina dhidi ya Israel.
Mwaka 2001, Sharon alishinda uchaguzi mkuu baada ya kuwaahidi waisraeli kuwa angekabiliana vilivyo na mashambulizi yoyote kutoka kwa waplestina. Lakini uhasama ulikithiri na Sharon akachoka kuwa mvumilivu kwa wapalestina

TAARIFA HII NI KWA MUJIBU WA MTANDAO WA BBC
No comments:
Post a Comment