Mtoto mwenye ulemavu wa viungo ambaye hana mikono yote miwili na mguu
mmoja, anayetoka jamii ya kifugaji,bw Joseph Nyange(13),huenda
akaondokana na mateso ya muda mrefu yanayo mkabili baada ya kupata
wafadhili waliojitolea kumpeleka nchini Marekani kwa ajili ya
kuwekewa viungo bandia.
Bw Nyange aliyekuwa akilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Living
Water Children Center,kilichopo Kimandolu jijini hapa,ameondoka jana
kwenda nchini Marekani akiwa na matumaini makubwa ya kurejea kama
binadamu wengine.
Kabla ya hapo maisha yake yote yalitegemea zaidi kusaidiwa kwa kila
jambo ikiwemo kujisaidia,kula,kutembea,kuoga na hata kuvaa,hali ambayo
ilikuwa mzigo kwa mlezi wake.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa kituo hicho,bw ,Anzaamen
Kimaro alisema kuwa Nyange anayesoma darasa la tano,katika shule ya
msingi Mkini jijini hapa,aliletwa kituoni hapo mwaka 2009 akiwa na
umri wa miaka minne akitokea wilayani Simanjiro alikokuwa akiishi na
wazazi wake.
Alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa na ulemavu huo na kwamba
aligunduliwa na wasamalia wema waliomwona akiwa katika hali hiyo,
ndipo walipomleta katika kituo hicho,ambapo walimpokea na kuendelea
kumlea hadi alipofikia umri wa miaka 13 .
Alisema wazazi wa mtoto huyo wanamaisha ya chini na hawana uwezo wa
kumsaidia,hivyo kitendo cha wasamalia kumwopoa mikononi mwa wazazi
wake huenda kilisaidia kuokoa maisha ya mtoto huyo ,kwani historia
inaonyesha kwamba baadhi ya koo za kifugaji haziwezi kuishi na mtoto
mwenye ulemavu zikiamini kuwa kuzaa mlemavu ni kukaribisha nuksi ndani
ya familia.
Bw,Kimaro anawashukuru wafadhili wa kimarekeni waliojitokeza kumsaidia
kwa gharama zao kwenda nchini marekani kwa ajili ya kupatiwa viungo
bandia vitakavyomsaidia kupata uwezo wa kutumia mikono na mikuu yake
kama binadamu wengine wa kawaida.
‘’tuna mshukuru sana mungu kwa mapenzi yake aliyoyaonyesha kwa
wafadhili hawa waliojitokeza kituoni hapa kumsaidia huyu mtoto na leo
ndio anaondoka kwenye nchini Marekani kwa ajili ya kupata viungo
bandia’’alisema Kimaro
Aidha alisema kituo chake chenye jumla ya watoto 173 kimekuwa
kikipokea watoto mbalimbali kutoka mikoa tofauti hapa nchini,wakiwemo
wenye ulemavu wa viungo ambapo changamoto kubwa ni jinsi ya kumudu
kuwahudumia watoto hao ,kwani hakuna wahisani wa moja kwa moja zaidi
hutegemea nguvu zao binafsi katika kuendesha kituo hicho.
Alitoa wito kwa wadau ,wasamalia na mashirika mbalimbali hapa
nchini,kutumia faida kidogo wanayoipaka katika kuwasaidia watoto wasio
na wazazi kwani hakuna mwenye jukumu hilo hapa nchini bali kila mmoja
anawajibu wa kutoa chochote anachoweza kwa ajili ya kufanikisha maisha
ya watoto hao ambao nitaifa la Leo.
Naye mtoto Nyange pamoja na kukishukuru kitu hicho cha Living Water
Children Center kwa kumfikisha hapo alipofikia,alitoa wito kwa
watanzania kujenga utaratibu wa kusaidia wenye ulemavu na kuacha
kuwatenga.Alimshukuru mungu kwa wafadhili waliojitokeza kumsaidia
No comments:
Post a Comment