Katika salamu zake za rambirambi ambazo alizituma usiku wa jana, Jumatatu, Januari 13, 2014, kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, Rais Kikwete amesema kuwa amepokea taarifa cha kifo cha Bwana Liundi kwa masikitiko na huzuni.
“Bwana Liundi alikuwa mtumishi mtiifu wa umma, alikuwa mchakakazi wa kuaminika na alikuwa mwandishi hodari wa sheria. Tutamkubuka kama mtumishi mwadilifu na mwaminifu wa umma na mfano wa kuigwa wa utumishi bora,” amesema Rais Kikwete katika salamu zake za rambirambi na kuongeza:
“Nakutumia wewe Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi salamu zangu za rambirambi, nikiungana nawe kuomboleza kifo cha Bwana Liundi. Aidha, kupitia kwako nawatumia wanataaluma wote ya sheria nchini salamu nyingi za rambirambi kwa kuondokewa na mwenzao.”
Ameongeza: “Napenda vile vile kupitia kwako unifikishie pole nyingi kwa ndugu, jamaa na wanafamilia wa Marehemu Liundi ukiwajulisha kuwa niko nao katika masikitiko na majonzi ya msiba huu mkubwa. Wajulishe kuwa naelewa machungu yao katika kipindi hiki na namwomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na subira kuweza kuvuka kipindi hiki kigumu. Aidha, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, ailaze peponi roho ya Marehemu George Liundi. Amen.”
Ends
No comments:
Post a Comment