Monday, January 20, 2014

ADEBAYOR KIBOKO, AFUNGA MABAO MAWILI YA UKWELI

Emmanuel Adebayor wakati wa mechi yao na Swansea
Adebayor alifunga bao la kwanza kunako dakika ya 34, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 70.

Wachezaji wa Swansea walichanganyikiwa pale Tottenham ilipoimarisha mashambulizi hadi kumfanya Chico Flores kujifunga mwenyewe.

Swansea ilipata bao lake la kuvutia machozi kupitia kwa mchezaji wake Wilfried Bony.

Tottenham sasa ina alama 43 na inashikilia nafasi ya tano kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier.

Tangu Andre Villas-Boaz alipofutwa kazi tarehe kumi na sita Desemba mwaka uliopita, kama kocha wa Tottenham, Adebayor amekuwa akiandikisha matokeo ya kuridhisha.

Wakati wa uongozi wa Villas-Boaz, mchezaji huyo kutoka Togo, alikuwa hana nafasi katika kikosi cha Tottenham, lakini Tangu Sherwood, alipotwaa uongozi wa klabu huyo, mchezaji huyo amefunga magoli sita baada ya kucheza mechi nane. (BBC)


No comments:

Post a Comment