Wednesday, August 07, 2013
MOTO WATEKETEZA UWANJA WA NDEGE KENYA
Moto mkubwa umetokea katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta ulioko jijini Nairobi. Kwa sasa moto huo umeweza kudhibitiwa
Rais Uhuru Kenyatta amewasili katika uwanja huo na anatarjiwa kuhutibia waandishi wa habari baadaye. Hadi kufikia sasa hakuna ripoti zozote za majeruhi .
Mwandishi wa BBC katika uwanja huo amesema kuwa kulikuwa na moshi mkubwa uliotoka katika eneo la kuondokea na kuingilia wageniMamlaka ya uwanja huo imesema kuwa tayari watu waliokuwa katika eneo hilo wameondolewa.
Imesema kuwa baadhi ya operesheni za uwanja huo zimekatizwa huku ndege zinazoingia katika uwanja huo zikielekezwa kutua katika viwanja vingine ndege kama vile Entebe, Dar es Salam ,Kigali, Mombasa na kwingineko nchini KenyaBaadhi ya safari za ndege kutoka uwanja huo pia zime-ahirishwa.
Mwishoni mwa wiki jana baadhi ya wenye maduka ya Duty Free katika uwanja huo walifurushwa baada ya serikali kusema kuwa leseni za wenye maduka zilikuwa zimepitwa na muda.
Hata hivyo chanzo cha moto bado hakijabainika wakati uwanja huo ukifungwa kwa muda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment