Sunday, August 04, 2013

DROO YA NYUMBA YA AIRTEL KUCHEZESHWA

Jumapili 4 Agosti 2013, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel itachezesha droo ya kwanza ya mwenzi ya promosheni ya Shinda nyumba na Airtel Yatosha siku ya jumatatu 5th August 2013 inayokusudia kumtafuta mshindi wa nyumba ya kisasa iliyoko kigamboni jijini Dar es salaam.

Akiongea kuhusu droo hiyo meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema “Airtel kupitia promosheni ya Airtel yatosha inaendelea kuwazawadia wateja zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu kiasi cha shilingi millioni moja kila siku.”

Mpaka sasa zaidi ya wateja 21 wamejishindia na kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 21 kimeshatolewa na bado kuna nafasi kwa wateja zaidi ya 69 kuondoka na kitita cha shilingi million moja kila siku



Meneja huyo aliendelea kusema mbali na zawadi ya shilingi milioni moja Airtel pia inatoa zawadi ya kila mwenzi kwa mshindi wa mwenzi ambapo nyumba tatu za kisasa zimejengwa kwa na shirika la nymba la NHC katika maeneo ya kigambopni jijini Dar es salaam tunayo zawadi kubwa ya kila mwenzi kwa mshindi wa mwenzi ambayo ni zile nyumba 3 za kisasa zilizojengwa na wenzetu wa shirika la nyumba la taifa NHC zilizoko katika maeneo ya kigamboni jijini Dar es saalam, sasa droo yetu ya kumsaka mshindi wa nyumba ya kwanza itachezeshwa siku ya Jumatatu tarehe 5 mwenzi Agosti ambapo tutashuhudia mshindi atakayejinyakulia nafasi ya kujishindia makazi haya ya kisasa”.

“Natoa wito kwa wateja ambao bado hawajajiunga huduma ya Airtel yatosha kujiunga kwa kupiga*149*99# na kununua kifurushi cha wiki, siku au mwezi na kuunganishwa mojakwamoja kwenye promosheni na kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ya kuibuka mshindi wa nyumba au pesa taslimu kila siku”aliongeza Jackson

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Shirka la nyumba la NHC Yahaya Charahani alisema” nyumba zimekamilika na zipo tayari kukabidhiwa kwa washindi, tunaamini mshindi atakayepatikana atafurahia mandhari mazuri,mazingira na nyumba yenye ubora wa kiwango cha juu. Nachukua nafasi hii kuwahimiza watanzania wapate muda wa kutembelea nyumba hizi ili nao wapate nafasi ya kuona miradi mbalimbali tuliyonayo ambayo imelengwa kwaajili ya matumizi yao.

promosheni ya Airtel yatosha ilizinduliwa mwanzoni mwa mwenzi Julai kwa lengo kuwazawadia wateja wanaotumia huduma ya Airtel yatosha, mpaka sasa wateja kutoka mikoa mbalimbali wameibuka kuwa washindi kila siku tumepata washindi kutoka mikoa ya Dar es salaam, singida, Dodoma, Lindi, Mtwara, Arusha, Moshi,Sengerema,Katavi,Kagera(Ngara),Dodoma na bado tunapata washindi wengi zaidi kila siku. promosheni hii itadumu

kwa muda wa mienzi mitatu ambapo washindi zaidi ya 100 na nyumba 3 za kisasa zitazawadiwa hadi kufika mwisho wa promosheni hiyo.

No comments:

Post a Comment