Tuesday, July 09, 2013

LAURYN HILL AANZA JANA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MIEZI 3





Lauryn Hill akielekea jela kuanza kutumikia kifungo cha miezi mitatu jana 8/07/2013

Mwimbaji  maarufu katika ulimwengu wa hip hop Lauryn Hill, ambaye pia aliwahi kuwa katika kundi la Fugees pamoja na wasanii Pras na Wyclif Jean, jumatatu(jana) alikwenda jela kuanza kutumikia kifungo cha miezi mitatu kwa kosa la kukwepa kulipa kodi mapato.


Mwanamuziki huyo ambaye pia ni mama wa watoto watatu alikubali kosa mwaka jana kwa kushindwa kuweka rekodi za kodi ya mapato kwa zaidi ya dola za kimarekani milioni 1.8 kutokea mwaka 2005 mpaka 2007.

Mshindi huyo wa tuzo za Grammy alihukumiwa kwenda jela kwa miezi mitatu, ambapo atakuwa katika jela ya wanawake ya Danbury, iliyoko Connecticut, nchini Marekani.

Hill ameshauza jumla ya zaidi ya nakala milioni 16 za albam yake, lakini alipofika mbele ya jaji mwezi mei, 2013 alisema “niniaishi kawaida sana ukifananisha na kiasi cha pesa ninazozalisha kufaidisha wengine”

“Kuna mtu kapiga hesabu zake na kufikia kuwa nadaiwa dola milioni 600” alidai Lauryn Hill. “Niko mbele yako hapa najaribu kutafakari jinsi ya kulipa deni? Na kama haitoshi huo si utumwa, sijui” alimaliza Hill

Mfungua mashtaka alidai kuwa kiwango hicho cha hela kwa kiasi kikubwa kimetokana na mapato ya mauzo ya muziki anaoimba Lauryn Hill pamoja na mirabaha ya sinema aliyolipwa na makampuni mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2005 mpaka 2008.

Kwa mujibu wa mfungua mashtaka, hukumu ilitolewa “pia ikijumuisha kodi ya pato la ziada la mwaka 2008 mpaka 2009 ambapo pia alishindwa kuweka rekodi zake, pamoja na deni lake la kodi la New Jersey, ambapo jumla ya pato lake ni kiasi cha dola za kimarekani milioni 2.3 na kodi yake kuwa karibu dola za kimarekani 1,006,517”

Baadda ya kumaliza kifungo chake cha miezi mitatu, Hill ataendela kutumikia kifungo cha miezi mitatu cha kutokutoka nyumbani kwake, na mwaka mzima akiwa anachunguzwa tabia yake. Atatakiwa pia kulipa faini, kodi anazodaiwa na pamoja na kodi ya dola za kimarekani 60,000.


No comments:

Post a Comment