Tuesday, July 30, 2013

KIKONGWE CHAMBAKA MWANAFUNZI DARASA LA TANO

MWANAFUNZI wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 11 katika Shule ya Msingi Mjini Musoma, anadaiwa kufanyiwa  kitendo cha kinyama kwa kubakwa na kujeruhiwa vibaya katika sehemu zake za siri na babu wa miaka 65 mkazi wa mtaa wa Kawawa katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Wakizungumza wakiwa nje ya Hospitali ya Mkoa wa Mara, baada ya kumpeleka mtoto huyo kupata matibabu, wazazi wa mtoto huyo majina yanahifadhiwa  wakiwemo majirani na viongozi  wa Kataya Mwigobero, walisema mtoto huyo amefanyiwa kitendo hicho cha kikatili kwakudanganywa kupewa sh. 1,000 kila siku na mzee huyo kabla ya kufumaniwa na mmoja wa Askari Polisi wa Kituo Kikuu cha mjini Musoma.


Mama mlezi wa mtoto huyo, Asha Athuman akizungumza kwa uchungu alisema alishangazwa na mabadiliko makubwa ya tabia ya binti huyo, huku akipata taarifa kutoka kwa watu kuwa mtoto wake huenda na fedha shuleni mara kwa mara.

“Binti yangu amekuwa namabadiliko makubwa hasa akiwa anatembea,lakini pia nimekuwa nikielezwa kuhusu mtoto wangu kwenda na fedha shuleni wakati mimi simpi fedha hizo.

“Nilipopata taarifa hizo nilimwambia mfanyakazi wangu wa ndani kumfanyia uchunguzi, ndipo juzi jioni aliponiambiakuwa mtoto anamahusiano ya kimapenzi na huyu mzee na kwamba amemuita nyumbani kwake, tulipokwenda tukakuta wako chumbani hivyo nilimwita mume wangu ambaye ni polisi, alifika na kuvamia chumbani aliwakuta wako uchi wa mnyama,” alisema mama huyo huku akibubujikwa na machozi.

Hata hivyo mama huyo alisema baada ya kumpeleka mtoto hospitalini walibaini kuharibiwa vibaya katika sehemu zake za siri, huku mbakaji huyo akidaiwa pia kumwingilia kinyume namaumbile yake, jambo ambalo limemsabishia maumivu makali.

“Inaniuma sana kumbe ndiyo maana watu wanachukua uamuzi wa kujiua au kumpiga mtu risasi, hivi unawezaje kumbaka mtoto wa mtu mbele na nyuma kwa umri huu hadi unamfanyia maumivu makali hivi…tena cha kushangaza mbakaji amekamatwa baada ya muda mfupi, polisi wamempa dhamana je hapa kuna haki kweli au kwa vile mume wangu ni askari wa cheo cha chini, ingekuwa mtoto wa RPC kabakwa kweli huyu mtu asingeachiwa kwa muda huo?” alihoji mama huyo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mwigobero anakoishi mtoto na mtuhumiwa huyo wa ubakaji, Musa Kirenge amelaani kitendo hicho cha ukatili, ambacho amefanyiwa mtoto huyo na kutaka hatua kali za
kisheria zichukuliwe dhidi ya muhusika.

“Kitendo hiki kinapaswakulaaniwa vikali, lakini pia nasikitishwa na polisi kumuachia mtuhumiwa kwa dhamanaya haraka haraka kiasi hiki hadi inatia shaka…namuomba RPC kupitia kwa OCDkumrejesha mtuhumiwa ndani, wakati taratibu nyingine za kisheria zikifuata kwani jamii imechukizwa na kitendo hiki, hivyo wanaweza kuchukua sheria mkononi kwa kumvamia na kumuua mtuhumiwa,” alisema diwani huyo.

Naye mtoto huyo kwa ina limehifadhiwa, alisema mzee huyo amekuwa akimfanyia vitendo hivyo vya kikatili mara kwa mara kwa kumuita ndani ya moja ya chumba cha nyumba yake, kisha kumpatia fedha za kununulia vitumbua shuleni, huku akimtishia kumuua endapo angetoa taarifa hizo kwa wazazi wake.

Mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mara, amewaambia waandishi wa habari kwa masharti ya
kutotajwa  kwamba, mtoto huyo amefanyiwa ukatili huo mkubwa na kwamba leo, wanatarajia kumpima kipimo cha mwisho cha kuangalia kama kaambukizwa virusi vya UKIMWI au la.

Jeshi la Polisi mjini Musoma nalo limethibitisha kutokea kwa tukiohilo na kwamba, linasubiri taarifa rasmi za madaktari kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi za kisheria.

No comments:

Post a Comment