Mji wa Arusha umekumbwa na tafrani ikiwa ni siku ya tatu
toka kutokea mlipuko wa bomu lililouwa watu wa tatu na watu zaidi ya 70
kujeruhiwa katika lala salama ya kampeni za uchaguzi wa madiwani eneo la
Soweto.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limelazimika kutumia mabomu ya machozi pamoja na risasi za moto kutuliza ghasia zinzoendelea jijini Arusha.
Mmoja wa walioshuhudia vurugu hizo aliyejitambulisha kwa
jina la Baba Enoki, mkazi wa Sakina mfanyakazi wa kituo cha kuuza mafuta cha Njake,
kilichopo Soweto alidai kuwa “Toka asubuhi kati ya saa tatu na saa nne, mahema
yalikuwa yanafungwa katika hali ya utulivu tu”,
“Ulinzi ulikuwa umeimarishwa kwani walikuwepo polisi wengi
sana lakini walikuwa mbali na wananchi”alieleza Baba Enoki.
“ Kwenye muda wa saa nane msafara wa viongozi wa CHADEMA
wakaingia Soweto na kupanda kwenye gari la matangazo la CHADEMA, wakahutubia
hali ikabadilika” aliongeza.
Baba Enoki anadai gari la matangazo la CHADEMA liliposogelea
watu ndipo vurugu zilipoanza na mabomu ya machozi na risasi za moto
ziliporindima kwa wakati mmoja. Wananchi walilazimika kuanza kukimbia huku na
kule kusalimisha maisha yao.
Katika tafrani hiyo, baadhi wakianguka ikiwa ni pamoja na
watoto na wanawake, polisi waliwakama na kuwapiga huku wakitoa matusi na maneno
ya kashfa huku wakiwaburuza na kuwaingiza kwenye karandinga la polisi.
“Nimeshuhudia kwa macho yangu mwenyewe polisi wasiopungua
sita wakiwaburuza watu huku wakiwapiga mateke na kuwapandisha kwenye gari”
alieleza mfanyakazi huyo.
“Baada ya kuondoka nao, polisi wengine muda si mrefu wakaja
na maboksi wakawa wanaokota vitu na kuweka kwenye maboksi hayo na kisha
kuondoka nayvo” aliongeza Baba Enoki
Kutokana na kitendo hicho ndipo wananchi wakaanza kuwatupia
mawe polisi huku polisi wakirudisha mabomu ya machozi na risasi za moto
“Aksari waliendelea kupiga mabomu huku wakivunja vioo vya
magari na kuharibu mali za watu mitaani.”
Hata hivyo wananchi waliamua kuchoma matairi na kujaza mawe
barabarani kwa lengo la kufunga barabara ya Moshi Arusha, polisi wameendelea
kukakamata pikipiki na kuzirundika katika viwanja vya Soweto.
No comments:
Post a Comment