Habari za
kusikitisha na pigo kubwa kwa wapenzi wa sinema duniani pamoja na wale
wanaofuatilia ‘series’ tamthiliya haswa ile maarufu ya Sopranos wamekumbwa na
msiba mkubwa baada ya msanii maarufu wa tamthiliya hiyo kufariki dunia.
James
Gandolfini, anayeigiza kama kiongozi wa
genge na kujulikana kama Tony Soprano katika filamu hizo za televisheni ya HBO
"The Sopranos,"
alifariki ghafla leo akiwa na umri wa mikaka 51.
Kwa mujibu
wa taarifa zilizoripotiwa na mtandao wa Yahoo, Gandolfini alikuwa katika
mizunguko
jijini Rome, Itali katika mapumziko kabla ya kuelekea Sicily kwenye
tamasha la filamu maarufu kama Taormina Film Festival ambapo aliugua.
Kwa mujibu
wa Yahoo, taarifa zinazotatanisha zilizotolewa kueleza chanzo cha kifo chake
zilidai alikuwa na matatizo ya shinikizo la damu wakati taarifa nyinginze
zikidai alipooza.
Msemaji wa
televisheni ya HBO iliyoko Marekani ambao ndio wanaorusha vipindi vya Sopranos
alidhibitisha kwa kusema “tumeshtushwa na kusikitishwa sana na kifo cha
mwanafamilia mwenzetu. Aliheshimu kila mtu na kuwa mtaratibu sana na mtu mwenye
upendo”
“kwa namna
moja au nyingine alitugusa katika maisha yetu, kwa utani wake, upendo na utu. Mioyo
yetu inaungana na mkewe na watoto wake katika kipindi hichi kigumu. Atakumbukwa
sana katika familia yetu”
No comments:
Post a Comment