Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia mapema leo, afya ya aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Mzee Nelson ‘Madiba’ Mandela imezidi kuwa
mbaya. Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amedhibitisha hayo alipomtembelea hospitali
jana na kuzungumza na mke wa Mzee Mandela, pamoja na timu ya madaktari.
SOMA ZAIDI...
Rais Zuma alieleza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa ‘Madaktari wanafanya kila kinachowezekana kumsaidia kurudi katika hali yake ya kawaida’
Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Nelson Mandela mwenye
miaka 94, alipelekwa hospitali huko Pretoria mwanzo wa mwezi juni ikiwa ni mara
ya tatu mwaka huu, Mandela amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kupumua
Zuma alidai madaktari wamemweleza kuwa hali ya Mandela
inazidi kuwa mbaya sana na imekuwa hiyvo katika muda wa masaa 24 yaliyopita.
“Madaktari wanapambana kujitahidi kurudisha hali yake kuwa
kawaida na yuko chini ya uangalizi mzuri na katika mazingira mazuri. Madiba yuko
katika mikono mizuri” alieleza Rais Zuma, kwa kutumia jina la kikabila la
Mandela ambalo ndio maarufu sana Afrika Kusini.
Zuma
akifuatana na kiongozi wa chama kinachotawala cha African National
Congress (ANC), Cyril Ramaphosa wameomba maombi zaidi kwa Bw. Mandela na timu
yake ya madaktari.
Msemaji wa
Bw.Zuma, Mac Maharaj aliliambia shirika la habari la BBC kwamba "madaktari wametumia neno ‘hali mbaya sana’ inatosha kutuweka roho juu kuhusiana na
hali ya Madiba".
No comments:
Post a Comment