Nyota wa Hip Hop Rick Ross, anusurika kupoteza maisha baada ya kukoswa koswa na risasi kadhaa kwenye gari yake aina ya Rolls Roys zilizorushwa na mtu mmoja ambaye bado hajafahamika
Taarifa za polisi zinasema kuwa asubuhi ya jana wamepokea simu nyingi kutoka kwa wakazi ambao wanaishi maeneo ya Las Olas baada ya kusikia mlio wa risasi
polisi wanasema gari lingine lilisimama karibu na gari la nyota huyo na mtu mmoja aliekuwa ndani ya gari hilo kuanza kurusha risasi kwenye gari la Ross
Nyota huyo hakupatwa na risasi hata moja wakati wa tukio hilo na hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa ndani ya gari hilo.
Mpaka sasa hakuna alietuhumiwa, kugundulika wala kushikiliwa juu ya tukio hilo, polisi wanaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo
No comments:
Post a Comment