Saturday, July 14, 2018

TFS NA WADAU WAANZ ASAFARI YA KUTEMBELE A MSITU WA ASILI WA AMANI

 Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS),Mariam Kobelo akigawa Vipeperushi kwa Wakazi wa Dar es Salaam ambao wanafanya safari ya kutembelea Msitu wa Asili wa Amani uliopo tanga ,aSafari hiyo ambayo imeratibiwa na TFS imeweza kuwakutanisha wadau mbalimbali kwenda kujionea mazao ya Misitu
 Baadhi ya Wadau waliopo katika safari hiyo wakipitia majarida yanayoelezea Msitu wa asili wa Amani na Vivutio vyake.
 Baadhi ya Wanafunzi waliojumuika katika Safari hiyo wakisoma Makala mbalimbali zilizomo kwenye Jarida linalozungumzia Msitu  wa asili wa Amani.
  Baadhi ya Wadau waliopo katika safari hiyo wakipitia majarida yanayoelezea Msitu wa asili wa Amani na Vivutio vyake.
Wadau wakiw akatika basi tayari kwa ajili ya Safari kuelekea Tanga kutembelea msitu wa asili wa amani


Wednesday, June 27, 2018

TASUBA YATOA UFADHILI KWA WANAFUNZI WA KIKE 20 AFRIKA MASHARIKI



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imezindua mpango wa ufadhili wa masomo ujulikanao kama Sanaa tuition fee waiver scholarship kwa wanafunzi 20 kwa mwaka wa masomo 2018/2019.ambapo kwa upande wa Tanzania ufadhili huo utahusu wasichana 10 ,wanafunzi wengine kumi watatoka nchi wa washiriki wa jumuia ya Afrika Mashariki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo wilayani Bagamoyo, Mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye amesema “Taasisi imekuja na mkakati wa kutoa ufadhili wa ada ya masomo ili kuweza kuziba mapengo makubwa mawili ambayo yamedhihirika katika utoaji wa mafunzo. Kwanza kuna uwiano hasi kati idadi ya wanachuo wa kike na wale wa kiume.

 Wanachuo wa kike wanaodahiliwa kila mwaka na Taasisi ni wachache sana (chini ya 30%) ikilinganishwa na wa kiume. Pili, pamoja na kupata hadhi ya kuwa kituo cha ubora uliotukuka kwenye ufundishaji katika nyanja za utamaduni na sanaa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Taasisi haijaweza kudahili wanachuo kutoa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.”alisema Makoye

Aliongeza kuwa  malengo makuu ya utoaji wa Ufadhili wa ada ya masomo ni Kuwezesha vijana wa kike wa Kitanzania wenye vipaji vya sanaa kupata nafasi ya kunoa vipaji vyao kupitia kozi mbalimbali zinazotolewa kwenye Taaisisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). 

Lakini pia ni fursa kwa Taasisi kujitangaza nje ya mipaka ya Tanzania na kuingia katika soko  na kuuza bidhaa zake kwa raia wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki

Naye mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TaSUBa ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo Ndg.George Daniel Yambesi aliishukuru TaSUBa kwa ufadhili huo Kwa  kuwa  umeonyesha  njia, kwa sababu ni kweli kabisa kuwa kuna vijana wengi wenye vipaji hasa wa kike ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za masomo.

Aidha ndugu Yambesi aliitaka TaSUBa ihakikishe ufadhili huu kweli unakwenda kwa walengwa; yaani vijana wenye vipaji vya sanaa na wana uhitaji wa ufadhili. Kwa kufanya hivi matunda ya ufadhili huu yataweza kweli kuonekana baada ya vijana hawa kuhitimu masomo yao.

Wakati huo huo ,baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza zimejitolea kufadhili malazi na Chakula kwa kipindi chote cha masomo kwa wanafunzi kumi wa kike kutoka Tanzania watakao faidika na ufadhili huo.

Uzinduzi huo ulisindikazwa na onyesho la ngoma za asili kutoka TaSUBa na Muziki kutoka kwa Jhikoman na Afrikabisa
 Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TaSUBa  Ndugu George Daniel Yambesi ,akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
 Mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Francis Makoye  akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Bi.Edda Sanga akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
 . Mwenyekiti wa chama cha wabunifu mitindo Ndugu.Merinyo Desumbuka akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fisoo akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
 Mwakilishi kutoka Basata Ndugu Onesmo Kayanda akiongea wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ufadhili wa masomo.
 Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TaSUBa  Ndugu George Daniel Yambesi akibofya kitufe kuashiria uzinduzi wa ufadhili wa masomo.

 Onyesho la ngoma za asili kutoka TaSUBa
 Onyesho la Muziki kutoka kwa Jhikoman na Afrikabisa

 Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TaSUBa  Ndugu George Daniel Yambesi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa tasuba pamoja na waalikwa


Monday, June 11, 2018

KITUO CHA AFYA TAMOTA - BUMBULI VIJIJI 20 KUNUFAIKA


PICHANI: Moja ya majengo ya Kituo cha Afya Tamota, Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo January Makamba alikagua ujenzi wake jana Juni 10, 2018. (Picha na Yusuph Mussa, Immamatukio Blog).

Na Yusuph Mussa, 
Immamatukio Blog, 
Lushoto

WANANCHI wa vijiji zaidi ya 20 wanatarajiwa kunufaika na ujenzi wa Kituo cha Afya Tamota kilichopo Kijiji cha Tamota, Tarafa ya Bumbuli, Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Ni baada ya Serikali Kuu kutoa sh. milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa majengo muhimu kwa iliyokuwa Zahanati ya Tamota ili kuwa Kituo cha Afya.

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba jana Juni 10, 2018 alitembelea Kituo cha Afya Tamota kuona ujenzi unavyoendelea ambapo kwa sasa ujenzi wake umefikia hatua ya linta.

Baadhi ya majengo yanayojengwa ni wodi ya wanawake ikiwemo wazazi, maabara, upasuaji na nyumba ya mtumishi, ambapo hadi sasa ujenzi huo umegharimu sh. milioni 135.6

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Afisa Mtendaji wa Kata ya Tamota Sophia Matogolo alisema kati ya fedha hizo, wananchi wamechangia sh. milioni 10 ikiwa ni pamoja na kuchota maji na kuchimba msingi wa majengo hayo.

Katibu wa Mbunge ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kwamkomole, Hozza Mandia alisema kituo hicho kitamaliza matatizo ya wananchi kupata huduma za afya kwenye kata za Tamota, Mahezangulu na Funta katika Jimbo la Bumbuli.



Sunday, June 10, 2018

WAZIRI AAGIZA KUKAMATWA KIONGOZI ALIYEFUJA MILIONI 23


PICHANI: Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na kujionea ununuzi wa pamba, Picha Zote Na Mathias Canal, WK


Na Mathias Canal-WK, Singida

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Mrakibu wa polisi Wilaya ya Iramba ASP Magoma Mtani kumkamata aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha ushirika (AMKOS) Msai.

Waziri Tizeba ametoa agizo hilo jana 9 June 2018 Mara baada ya kutembelea kitongoji cha Kati, Msai na Mtoa akiwa katika ziara ya kikazi ya Siku mbili kwa ajili ya kutembelea vituo vya ununuzi wa pamba na kujionea msimu wa ununuzi wa zao hilo katika vijiji hivyo.

Dkt Tizeba amelaani vikali ufujaji huo wa fedha za wakulima huku akimtaja Paul Ramadhan Kurwa kuhusika na ufujaji huo wa shilingi milioni 23 huku akiendelea kuonekana mtaani pasina kuchukuliwa hatua za kisheria.

"Wakati muelekeo wa serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli ukijipambanua kutaka kuboresha maisha ya watanzania kupitia Kilimo lakini kuna watu wanataka kurudisha nyuma juhudi hizo, hakika tutawapa kibano kweli kweli hakuna utani kwenye fedha za wananchi" Alikaririwa Dkt Tizeba

Mhe Tizeba ametoa siku moja kukamatwa kwa mwizi huyo na kufikishwa mahakamani ili awe mfano kwa wezi wengine wasio kuwa na haya wala soni.

Aidha, amewataka wananchi katika msimu huu wa uuzaji na ununuzi wa Pamba kutouza Pamba zenye uchafu wakidhani wataongeza idadi ya kilo kwani kufanya hivyo ni kufifihisha juhudi zao wenyewe jambo ambalo halina tija.



Monday, June 04, 2018

ASKARI WA WANYAMAPORI WATAKIWA KUWA WAADILIFU NA MAKINI KUTOKANA NA WANYAMA WANOTOKA NJE YA HIFADHI


Na Mwandishi wetu

WALINZI wa wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori ya Akiba la Maswa yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wametakiwa kuwa makini na waadilifu kutokana na kuongezeka kwa wanyama adimu wanaofika maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA)
Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko alipokua akikagua shughuli za uhifadhi na ulinzi katika maeneo hayo.

Meja Jenerali Semfuko, alisema kazi ya kupambana na ujangili inahitaji uvumilivu, uadilifu na ujasiri mkubwa kutokana na mazingira hatarishi yaliyopo.

"La muhimu kuna taatifa maeneo haya wameanza kuja wanyama adimu hivyo ningependa muongeze jitihada hizi mara dufu wanyama hao wasidhurike," alisema.

Katika ziara hiyo wajumbe wa Bodi ya TAWA walipokea taarifa ya timu ya pamoja kati ya TAWA, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Frankfurt Zoological Society  ( FZS), TAWIRI na Friedkin Conservation Fund (FCF) katika kuhifadhi na kulinda na kuhifadhi wanyama adimu.

Taarifa hiyo iliyowasilishwa na wataalamu Philbert Ngoti wa TANAPA na Gerald Nyaffi wa FZS katika  eneo la kitalu kilichopo Maswa Mbono kinachoendeshwa na kampuni ya Tanzania Game    Tracker Safaris  (TGTS).

Wataalam hao walisema wamefanikiwa katika mradi huo kwa ufadhili wa familia ya Friedkin inayomiliki TGTS ililiyofadhili fedha, vifaa pamoja na helikopta, kazi ijayotarajiwa kuendelea katika maeneo mengine.

Katika ziara hiyo TAWA  imeridhishwa na utendaji wa Makampuni ya uwindaji na upigaji picha za kitalii, yaliyopo katika maeneo yake kwa kusimamia uhifadhi na ulinzi pamoja na kuchangia miradi ya maendeleo ya wananchi yenye thamani zaidi ya sh 40 bilioni.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Dk James Wakibara akizungumza na waandishi wa habari juu ya mchango kwa jamii, uhifadhi na kiuchumi wa  makampuni ya uwindaji wa kitalii zilizowekeza katika maeneo yao.

Maeneo yaliyotembelewa na TAWA ni pamoja  na Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori(WMA) ya Makao wilayani Meatu inayosimamiwa na kampuni ya Mwiba Holdings Limited.


Dk Wakibara alisema, licha  mchango wa makampuni kwenye jamii, pia TAWA kupitia malipo  ya kampuni hizo, imekuwa ikitoa  takriban sh 6.5 bilioni kila mwaka kwa vijiji vyenye wawekezaji hao na halmashauri.


Makampuni hayo yamewekeza katika baadhi ya maeneo ya vitalu 159   vilivyopo nchini na maeneo ya hifadhi za jamii za wanyamapori (WMA) 38 zilizopo nchini.


"Hizi kampuni za kitalii zina mchango mkubwa sana pia katika uhifadhi wa maeneo haya, hasa katika vita dhidi ya ujangili ikizingatiwa asilimia 95 ya maeneo yaliyohifadhiwa nchini yapo chini ya TAWA"alisema


Alisema kwa sasa mapato ya TAWA kutokana na shughuli za uhifadhi, yamefikia dola 20 lakini kuna mikakati ya kuongeza mapato hayo mara nne zaidi hadi kufikia dola 80.


"kuna dhana potofu kuwa uwindaji wa kitalii ni kumaliza wanyama hili sio kweli, kwani haya makampuni hayajawahi kufikia hata robo  kiwango cha kuwinda wanyama ambacho kinatolewa kila mwaka na TAWA na mashirika ya kimataifa"alisema


Mwenyekiti wa bodi ya TAWA, Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko alisema mamlaka hiyo ipo katika mabadiliko  makubwa ili kuhakikisha jamii inanufaika zaidi ya uhifadhi wa wanyamapori,katika kusaidia miradi ya kijamii ya maji, afya Elimu na uhifadhi.


Mwenyekiti huyo na bodi yake ambao walitembelea pori la Makao, lilipo mpakani mwa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Meatu,alisema wameridhishwa na utendaji wa kampuni ya Mwiba Holding katika eneo hilo
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA)
Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko, Akikagua Gwaride la Askari wa Wanyamapori wa pori la akiba Maswa.
 Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA)
Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko akiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa Wizara  ya Maliasili washirika wake


Sunday, June 03, 2018

MAPACHA WALIOUNGANA CONSOLATA NA MARIA WAFARIKI DUNIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali watoto wawili Mapacha walioungana Maria na Consolata ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.


Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa na kifo cha mabinti mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti waliofariki dunia jana jioni katika hospitali ya Mkoa wa Iringa.

Mhe. Rais Magufuliwa aliwatembelea Maria na Consolata walipokuwa wakipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam tarehe 06 Januari, 2018.

Pamoja na kuwapa pole Maria na Consolata waliongoza sala ya kuliombea Taifa na Viongozi wake.



Saturday, June 02, 2018

MTAJI WA BENKI YA TPB UMEKUWA KUTOKA BILIONI 8 HADI BILIONI 60

 
Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki hiyo,Proffesa Lettice Rutoshobya akifungua tawi jipya la TPB mkoani Tanga kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi akishuhudia


Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki hiyo,Proffesa Lettice Rutoshobya akikata utepe kushiria ufunguzi wa tawi la TPB Tanga kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi na kulia ni Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB Dkt Edmund Mndolwa


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB Dkt Edmund Mndolwa amesema mtaji wa benki hiyo hivi sasa umekuwa kutoka Bilioni 8 hadi kufikia Bilioni 60 hatua inayoonyesha utendaji mzuri wa wafanyakazi kutokana na kutoa huduma bora zinazowafanya wateja kuvutiwa na kujiunga nao.

Dkt Mndolwa aliyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa tawi la Tanga la Benki hiyo lililopo eneo la Chumbageni Jijini Tanga ambao ulifanywa na Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Proffesa Lettice Rutashobya kwenye halfa iliyofanyika mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa bodi ya wakurugenzi na wafanyakazi.

Alisema hatua hiyo inatokana na huduma nzuri inayotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo na hivyo kusaidia kuwepo kwa ongezeko kubwa la wateja jambo ambalo limepelekea kuongezeka matawi nchini kutoka 32 mpaka 74 kwa sasa.

“Niwapongeze sana TPB kwa kasi kubwa ya utendaji mzuri mliokuwa nayo na kupelekea kuwezesha kupanua wigo wa matawi kwa wateja wenu ambapo awali kulikuwa na matawi 32 lakini hivi sasa yamefikia 74 hii ni hatua nzuri sana hivyo kuwatake muendelee nayo “Alisema.

“Lakini pia nimpongeze Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi anayemaliza muda wake Proffesa Lettice kwa kazi nzuri aliyoifanya jambo ambalo limewezesha kufikia mafanikio yaliyopo hivi sasa ndani ya benki hii nitaendelea kushirikiana na wafanyakazi “Alisema.



RC AAGIZA KOROGWE KUWA NA STENDI MOJA YA MABASI


PICHANI: Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe kwenye kikao na wadau wa Korogwe juu ya hatma ya matumizi ya stendi mbili katika Mji wa Korogwe. Kikao hicho kilifanyika jana Juni mosi, 2018 kwenye Ukumbi wa Halmashsuri ya Mji Korogwe (Picha na Yusuph Mussa).

Na Yusuph Mussa, Korogwe

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela ametengua maamuzi ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Korogwe ya kuruhusu kutumika kwa stendi mbili katika Mji wa Korogwe.

Na badala yake, ameagiza stendi itakayotumika ni ile ya Kilole ambayo Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli aliifungua Agosti 7, 2017, na kuachana na stendi ya zamani ya Manundu.

Aliyasema hayo jana Juni mosi, 2018 kwenye Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe na kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo madiwani, wakata tiketi za mabasi, wafanyabiashara, watumishi na kamati za ulinzi na usalama za wilaya ya Korogwe na mkoa wa Tanga, na kufanya mikutano ya hadhara kwenye stendi hizo.

Pamoja na marufuku hiyo ya stendi ya zamani, pia ameagiza vituo vya maegesho ya magari kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam kwenda Arusha kuanzia Mtonga, Mwembeni, Uwanja wa Sokoni, CRDB, Majengo na Kilole viondolewe.

"Kuanzia tarehe ya leo (Juni mosi) stendi ya mabasi itakuwa moja nayo ni Kilole. Na hiyo ni kutokana na kuongeza mapato ya Halmashauri ya Mji Korogwe. Lakini ni lazima turejee kwenye makusudio yetu ya kujenga stendi mpya, nayo ni kukidhi mahitaji ya wananchi kuweza kupata eneo nzuri na la kisasa katika kutoa huduma.

"Uwepo wa stendi ya zamani (Manundu) kufanya kazi, kunaharibu utaratibu tuliojiwekea, kwani badala ya mabasi kuingia Stendi ya Kilole, yanabaki stendi ya zamani, hivyo kuathiri ufanyaji wa shughuli kwenye stendi mpya. Lakini pia stendi zote zilizopo pembeni ya barabara kuu ziondolewe, zinachangia abiria na mabasi kutoingia stendi mpya" alisema Shigela.

Shigela alisema Stendi ya Manundu itumike kama daladala kwa magari yanayotoka kwenye kata za Halmashauri ya Mji Korogwe, bodaboda na bajaj na si vinginevyo, kwani hata idadi ya magari yanayoingia stendi ya zamani iliyoelezwa na madiwani kuwa hayazidi 10, siyo ya kweli, kwani zaidi ya magari makubwa 40 yanaingia stendi ya zamani kwa siku.



DKT. KIGWANGALLA ASHIRIKI MAZISHI YA MAMA MZAZI WA HUSSEIN BASHE NZEGA


Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimfariji mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake mzazi aliyezikwa leo wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye. Wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Abdallah Bulembo wameshiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.


Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimfariji mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake aliyezikwa leo wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na mbunge wa Kigoma Vijijini, Peter Selukamba. Wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Abdallah Bulembo wameshiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.