Pages

Tuesday, April 08, 2014

EDWARD LOWASA ATOA MSAADA MWINGINE, SOMA HAPA

Iringa

Waziri Mkuu mstafu  Edward Lowasa ametoa msaada wa chakula kwa ajili ya kumaliza arobaini ya aliyekuwa shekhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa Marehemu Alhaji Ali Juma Tagalile iliyofanyika juzi Nyumbani kwake mjini Iringa.

Shekhe Tagalile alifariki dunia Machi 6 mwaka huu katika hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa alikokuwa amelezwa kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu. Lowasa ambaye hakuhudhuria hitima hiyo iliyoambatana na kusomwa kwa dua alitoa msaada wa vyakula kupitia kwa mwakilishi wake Fadhili Ngajilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Ngajilo ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa alisema Lowasa ametoa msaada huo kutokana na mahusiano mazuri aliyokuwa nayo na marehemu wakati wa uhai wake.


“Mh.Lowasa alisema ameamua kutoa msaada huu kama sehemu yake ya kumlilia Marehemu Tagalile kutokana na uhusiano mzuri waliokuwa nao wakati wa uhai wake,alifanya nae kazi vizuri na pia alikuwa mshauri kwa mambo mengi”alisema Ngajilo.

Akitoa shukurani zake kwa tukio hilo msemaji wa familia ya Marehemu, Said Tagalile ambaye pia ni mdogo wa marehemu alimshukuru mh. Lowasa kwa msaada wake na kuongeza kuwa umesaidia kufanikisha shughuli hiyo muhimu.

“Sisi kama wanafamilia tumefarijika na sadaka hii,tunawashukuru watu wote waliojitokeza kutufariji na pia tunamshukuru Lowasa kwa kutupatia sadaka iliyofanikisha zoezi hilo muhimu tunamuombea kwa mungu pale alipopunguza mwenyezi mungu amuongezee"alisema Tagalile.

Said alitaja vitu vilivyotolewa na Lowasa kwa ajili ya kuhitimisha arobaini ya Shekhe huyo ambaye ni kaka yake kuwa ni  Gunia nne za Mchele,Ng’ombe mmoja na Ndoo mbili za mafuta ya kula  zenye ujazo wa lita 20 vyote vinadaiwa kugharimu kiasi cha Sh milion 1.5

Marehemu ambaye katika kipindi cha uhai wake alikuwa shekhe Mkuu wa mkoa wa Iringa pia amewahi  kujishughulisha na mambo mbalimbali ya kijamii kiuchumi na kisiasa. 

Said alitaja baadhi ya nyazifa alizoshika marehemu Tagalile wakati wa uhai wake kuwa ni pamoja na wenyekiti wa Bodi ya Msamaha wa Wafungwa Mkoa wa Iringa (Parole)Daktari wa magonjwa ya binadamu tangu enzi ya mkoloni na pia mshauri wa masuala ya kisiasa.


No comments:

Post a Comment