Waamuzi wanne kutoka Gabon, ndio watakochezesha mchezo wa
kimataifa kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mapharao wa Misri utakaofanyika
Jumamosi Juni 4, 2016 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni ni wa kutafuta nafasi
ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika
Gabon ambako mwamuzi wa kati atakuwa ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou
Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric.
Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo
ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la
Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia kesho Juni
mosi, 2016 ambako wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski,
Dar es Salaam.
Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko
katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei
30,2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars.
Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka
sare ya 1-1.
No comments:
Post a Comment