Wednesday, June 12, 2013

MFANYAKAZI WA NDANI AUAWA KIKATILI

8 WASHIKILIWA KWA UJAMBAZI DAR



JESHI la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, limemkamata mtunza bustani, Philimon Laizer (27), mkazi wa Mikocheni B, kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mfanyakazi mwe n z a k e wa n d a n i , Perepetua Mainabu (PICHANI JUU). Marehemu aliuawa
kwa kuchinjwa sehemu ya shingo, kumsababishia jereha sehemu ya mkono wa kushoto na kwenye paji lake la uso na mwili kutapakaa damu kichwani.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema tukio hilo lilitokea karibu na dampo la kutupa takataka pamoja na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Kamanda Kova alisema mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika na tukio hilo na kwamba ma r e h emu a l i o n d o k a nyumbani saa mbili siku ya tukio hadi siku ya Ijumaa ulipopatikana mwili wake akiwa umeuawa kikatili. Alisema jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa huyo.

Katika hatua nyingine Polisi jijini Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa nane kutokana na kujihusisha na matukio ya ujambazi. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema kundi hilo, lilikuwa baya na tayari lilikuwa linafanya matukio mbalimbali ya kuvizia raia wa China na wengine wa kigeni katika fukwe za Bahari ya Hindi na kuwapora mali zao.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Issaya Sakanga (31), Yusuf Juma (33) na wenzao ambao hakuwatajwa majina. Alisema watu hao walihusika kupora raia wa Sweden mkoba wake, Gusela Bergstrom.

Alitoa tahadhari kwa raia wa kigeni kuacha kutembea na fedha nyingi mikononi kwani ni hatari kwa usalama wao. Alishauri watumie njia nyingine ikiwa ni pamoja na kutumia wafanyakazi zao fedha kwa kutumia mitandao ya simu.

No comments:

Post a Comment