Tuesday, June 11, 2013

JUSTIN BIEBER AWEKA BRA KWENYE INSTAGRAM!



ATIMULIWA KLABU BILA KUTEGEMEA

 

Justin Bieber(JB) kwa uhakika si mtoto tena, sasa hivi ana mashabiki mpaka wengine wanamtupia brazia (JUU PICHANI) jukwaani. JB mwenye miaka 19 aliweka picha ya kivazi hico cha ndani cha wanawake kwenye mtandao wa kijamii wa instagram.


Brazia hiyo ya rangi ya pink ilirushwa na mmoja wa
mashabiki wake juzi jumapili (tarehe 9) alipokuwa kwenye shoo ya Believe.


JB aliweka picha hiyo na maelezo yake “I guess everyone grows up” akimaanisha nahisi kuwa kila mtua anakua.


Wakati mashabiki wa JB wamekua, gazeti la The Sun limeripoti kuwa msanii huyo alibadilika rangi ya uso alipotimuliwa kwenye klabu ya kujirusha na maarufu sana Los Angeles, Marekani iitwayo Lure's Toxic aLuau Beach Party ilipofika saa moja jioni kisa umri mdogo.

Gazeti hilo lilidai Bieber aligundulika baada ya rapa maarufu The Game kumgundua, ambapo chanzo kimoja kilieleza kuwa ‘mmoja katika kundi la Justin alitokea mapema na kudai kuwa Justin angekuja baadae’

‘wenye klabu wakasema hawatomruhusu kwasababu hana miaka 21. Lakini Bieber alikuja na kujaribu kuingilia mlango wa nyuma’ kilieleza chanzo hicho na kuripotiwa kwenye gazeti la The Sun.

Chanzo hicho kiliendelea ‘The Game alikuwa kwenye mic na ndipo alimuona Bieber akijaribu kuingia na kusema kwa nguvu Bieber anaingia ndani’
‘ndipo walinzi walipomuona na kumsindikiza nje mara moja. Akaondoka maramoja huku akijiskia vibaya’



No comments:

Post a Comment