Saturday, March 17, 2018

MHUDUMU ALIYEANGUKA TOKA KWENYE NDEGE UGANDA AMEFARIKI

Mhudumu aliyeanguka toka kwenye ndege (pichani kushoto) katika Uwanja wa Kimataifa wa Entebe, Uganda amefariki. Mwanamke huyo ambaye utaifa wake haujatajwa alikimbizwa katika hosptiali ya Kisubi, iliyoko umbali wa kilomita 16 toka eneo la tukio, na kufariki muda mchache baadae.

Kwa muujibu wa taarifa, mfanyakazi huyo wa Shirika la Ndege Emirates ambaye ni mhudumu wa kwenye ndege alikuwa maandalizi ya ndege kabla ya kuruhusu abiria kuingia kwaajili ya kuanza safari.

Taarifa za ajali hiyo zilisambaa katika mitandao ya jamii na kuzua hisia mbalimbali za sababu ya tukio hilo.

Shirika la Anga la Uganda limeanza uchunguzi ili kujua chanzo cha kifo cha mhudumu huyo. Taarifa zimeeleza kuwa mhudumu huyo “alifungua mlango wa dharura” na kwa bahati mbaya “akaanguka kutoka kwenye ndege hiyo iliyotua salama ikiwa imesimama”

Msemaji wa Hospitali ya Kisubi, Edward Azbonna aliliambia shirika la utangazaji la BBC kuwa mhudumu huyo alipatwa na majeraha usoni na katika magotini. Alieleza kuwa alizimia lakini ni mzima. Alifikishwa katika hospitali hiyo siku ya jumatano na kufariki muda si mrefu.

No comments:

Post a Comment