Friday, March 16, 2018

DARAJA LA WAVUKA KWA MIGUU LABOMOKA, LAUA 10 (PICHA)

 Watu kumi wamepoteza maisha baada ya daraja jipya la waenda kwa miguu kubomoka jana katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Florida(FIU), Miami, nchini Marekani.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la kila siku la Mail Online, daraja lenye urefu wa futi 174, lililojengwa ili kuhudumia waenda kwa miguu kutoka kampasi ya FIU kuelekea maeneo ya makazi ambayo baadhi ya wanafunzi wanaishi, liliwekwa jumamosi na kwamba halikuwa tayari kutoa huduma mpaka mwaka 2019.

Kwa mujibu wa CBS Miami, wafanyakazi wawili walikuwa wakiendelea na matengenezo katika daraja hilo liligharimu dola za Marekani milioni14(sawa na shilingi bilioni 31.6 za Tanzania), wakati linadondoka.

Seneta wa jimbo la Florida amedhitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema kuwa kati ya watu sita mpaka kumi wamepoteza maisha. Naye Meya wa Kaunti ya Dade-Miami, Carlos Gimenez amewaeleza waandishi wa habari kuwa angalau watu sita walitolewa katika tukio hilo huku magari nane yakiwa yamenasa chini ya daraja hilo.

Alieleza kuwa mtu mmoja alipatwa na mshtuko wa moyo. Chuo Kikuu cha Florida (FIU) kilitoa tamko likidai kushtushwa na kusikitishwa na tukio hilo. Angalia picha zaidi hapa. 













No comments:

Post a Comment