Thursday, March 15, 2018

AJIFUNGUA BAHARINI PICHA ZAZAGAA MITANDAONI (ANGALIA HAPA)


PICHANI : Daktari akiwa amebeba kichanga huku baba wa kichanga hicho akiwa amebeba mfuko wa uzazi kwenye bakuli la plastiki baada ya kichanga hicho, kushoto ni mama mtoto baada ya  kujifungulia baharini hivi karibuni.

Imetafsiriwa na Mwandishi Wetu
Immamatukio Blog

Picha za mwanamke anayedhaniwa kuwa raia wa Urusi zimesambaa mitandaoni zikimuonesha mama huyo baada ya kujifungulia mtoto baharini huku akisaidiwa na mtaalamu pamoja na mumewe hivi karibuni.

Mwanamke huyo ambaye anadaiwa kuwa ni raia wa Urusi alijifungua mtoto ambaye mpaka sasa hajajulikana jinsia yake na maendeleo yake. Picha za tukio hilo lililotokea nchini Misri, Dahab, mji ulioko maili 50 kasikazini mwa mji maarufu wa Sharm el-Sheikh zimesababisha wanawake wengi nchi za Ulaya kutamani kujifungulia baharini kama mama huyo.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la nchini Uingereza, mama huyo alijifungua kwa msaada wa Daktari kutoka Urusi, ambaye ni mtaalamu wa kuzalisha katika maji.

Picha zilizosambaa katika mitandao ya jamii, zinamuonesha Daktari na baba wa mtoto wakiwa wamebeba kichanga hicho wakitokea katika mawimbi, pwani Bahari Nyekundu (Red Sea) katika hotel ya kitalii mjini Dahab. Picha hizo zinamuonesha mtoto mchanga akiwa bado na kitovu hakijakatwa huku mfuko wa uzazi ukiwa kwenye chombo cha plastiki zilipigwa na mtalii aliyekuwa katika kibaraza cha hoteli.

Kwa mujibu wa shuhuda ambaye hakutaka kutambuliwa alisema Mama huyo akiwa na tumbo kubwa la ujauzito aliingia baharini akiwa amevaa nguo za kuogelea na baadae kutoka akiwa tayari ameshajifungua. Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook wamepongeza tukio hilo na kudai kuwa ni zuri na jepesi zaidi katika matukio ya kujifungulia kwenye maji.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Dahab, inadaiwa idadi ya wanawake wajawazito imeongezeka katika mji huo wakitamani kujifungulia baharini.

Mwanamke huyo, mumewe na kachanga chao hawakuweza kufahamika majina yao na hata kichanga hicho hakikuweza kujulikana jinsia au hali na maendeleo yake, kwani hakuna ripoti yoyote iliyoonesha tukio hilo.

Mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii aliandika “bahari ilikuwa nyekundu sana siku hiyo”

Dahab, mji ambao ulijulikana sana kwa shughuli za uvuvi, sasa hivi ni maarufu sana kwa utalii na kufahamika kama sehemu ya kivutio cha muhimu sana katika utalii wa kuzamia baharini.


No comments:

Post a Comment