Wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa nchini wameshauriwa kutumia fursa ya bure ya ukaguzi wa bidhaa zao inayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania TBS.
Hayo yamesemwa na Afisa Masoko Mwandamizi kutoka katika shirika hilo,Gladnes Kaseka (pichani kushoto juu) wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya tano ya biashara ya Mkoa wa Tanga .
Alisema kuwa licha ya TBS kutoa fursa hiyo lakini bado wazalishaji wadogo na wakati wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa ukamilifu wake na kusababisha kuendelea kuwepo kwa bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.
"Bado wazalishaji wetu wengi hawajaweza kuifikia fursa hiyo ambayo itaweza kuwasaidia kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora lakini wataweza kuingiza bidhaa zao kwa urahisi katika masoko ya ushindani tofauti na sasa" alisema Kaseka.

















