Thursday, June 23, 2016

WABUNGE KUSHIRIKI HARAMBEE YA MEDIA CAR WASH

Na MAELEZO

Zaidi ya waandishi wa Habari 1000 kutoka vyombo mbalimbali kunufaika na Mfuko wa Bima ya Afya kupitia msaada kutoka kwa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari.

PICHANI:  Mjumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari Bw. Peter Nyanje akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es Salaam kuhusu harambee ya kuosha magari itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni mjini Dodoma. Kushoto ni Mratibu wa Mratibu wa Media Car Wash Grace Nacksso   

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na mjumbe wa kamati hiyo Peter Nyanje wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambe ya maalum ya kuosha magari Media Car Wash for health itakayofanyika tarehe 25 Juni mjini Dodoma.

“Lengo la harambee hiyo ni kukusanya zaidi ya fedha takribani shilingi milioni 200 ambazo zitatumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi zaidi ya 1000 hapa nchini.”Alisema Nyanje.

Nyanje amesema kuwa harambe hiyo itakuwa ni yapili ikitanguliwa na ile iliyofanyika katika viwanja vya Leaders jijni Dar es Salaam na kufanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 30 ambazo zilisaidai kugharamia matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa taabani.
Aliongeza kuwa na harambee hiyo imekusudia kuhakikisha waandishi wengi zaidi wanakatiwa Bima ya Afya, ili kujikinga na kadhia ya kuchangiwa fedha pale wanapofikwa na maradhi.

Kwa upande wake Mratibu wa Media Car Wash Grace Nacksso ametoa rai kwa Wabunge, viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma kujitokeza kwa wingi katika katika viwanja vya Jamhuri ili kushiriki katika zoezi hilo ambapo watu wataoshewa magari yao na watu maarufu wakiwemo wasanii wa Bongo fleva ,Bongo Movie na Miss Tanzania Lilian Kamazima.

Grace amesema kuwa wao kama waratibu wa harambee hiyo wamejidhatiti kuhakikisha harambee hiyo inafanyikiwa ili kutimiza azma ya kusaidiana miongoni mwa wanataaluma ya habari nchini.

Harambe ya Media Car Wash itakayofanyika mjini Dodoma inatahudhuriwa na watu mashuhuri wakiwemo wasanii Joh Makini, Inspekta Haroun, Nikki Wa Pili, G. Nako, Aunt Ezekiel,Kajala Masanja, Ray Kigosi, Jacob Steven (JB) pamoja na Miss Tanzania Lilian Kamazima 

Msanii wa Bongo Fleva Inspekta Harun akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es Salaam kuhusu harambee ya kuosha magari itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni mjini Dodoma.Katikati ni Mjumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari Bw. Peter Nyanje. Kushoto ni Mratibu wa Mratibu wa Media Car Wash Grace Nacksso.


Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Wajumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Picha Zote na Frank Shija



No comments:

Post a Comment