Friday, February 05, 2016

KATIBU MKUU WA CCM AWATEMBELEA WAHADZABE NA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipozi kwa picha na Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe Chifu Edward Mashimba kushoto na Mama Sara Philipo mwenye nyumba hiyo wakati alipozungumza na chifu huyo leo, Katika ziara hiyo Kinana katika kijiji cha Kibampa na kukagua miradi mbalimbali ya jamii hiyo ya Kihadzabe ikiwemo maji, mabweni ya watoto wa jamii hiyo pamoja na zahanati iliyopo katika kijiji cha Munguli kata ya Mwangeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Ndugu Parseko Kone amewajengea mabweni na kuwawekea mradi wa maji, Umeme na kuwafundisha kilimo cha mihogo na mazao mengine ili kuweza kujikimu kwa chakula kwani jamii ya kabila hilo inakula nyama, mizizi ya miti na asali.

Lakini pia vijana hamsini wa Kabila hilo wamejiunga na jeshi la wananchi kwa mpango mkuu wa mkoa wa Singida Ndugu Parseko Kone na serikali kwa kuwaendeleza kielimu na kimaendeleo, kuna vijana wengine sitini wataingizwa jeshini ikiwa ni mkakati wa kuielimisha jamii hiyo ili kubadili maisha bila kuharibu mila yao.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MKALAMA -SINGIDA)



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe Chifu Edward Mashimba wakati alipotembelea na kujadiliana naye mawili matatu.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mama Sara Philipo mwenye nyumba hiyo wakitoka nje mara baada ya Kinana kuzungumza na Chifu Edward Mashimba.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe Chifu Edward Mashimba



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi hao wa jamii ya Wahadzabe huku Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe Chifu Edward Mashimba akitafsiri katika kijiji cha Kibampa kata ya Mwangeza.



Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akiwahutubia.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kazi ya kupanda mbegu ya muhogo na vijana wa Kihadzabe katika shamba darasa ililopo kijiji cha Kibampa kata ya Mwangezi ikiwa ni mafunzo ya kilimo kwa jamii hiyo.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya jamii hiyo wakati alipokuwa akiwasili kijiji cha Kibampa.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kucheza ngoma ya asili ya jamii ya Kihadzabe.



Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukikatisha misitu na mabonde wakati ukielekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa ambako jamii hiyo inaishi.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaklimiana na vijana wa kisukuma aliowakuta wakipalilia shamba, vijana hao walimweleza Kinana kuwa wanahitaji serikali iwatengenezee barabara yao jambo ambalo litarahisha hata uuzaji wa mazao yao.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa maji katika kijiji cha Munguli ambao umejengwa maalum kwa ajili ya jamii hiyo anayetoa maelekezo ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mabweni ya watoto wa jamii ya Kihadzabe yaliyojengwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone katika kijiji cha Munguli mabweni hayo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 60 wa kiume 30 na wakiume 30 yamejengwa maalum kwa ajili ya jamii kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai.



Baadhi ya wananfunzi wa shule hiyo



Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Munguli Athman Kinyere akisoma taarifa ya shule hiyo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana



Hii ni moja ya nyumba zinazotumiwa na jamii hiyo ya Kihadzabe.



Baadhi ya wananchi wa jamii hiyo wakiwa katika mkutano



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mtambo wa Sola unaoendesha maji katika mradi wa maji wa kijiji cha Munguli ambao umejengwa maalum kwa ajili ya jamii hiyo anayetoa


No comments:

Post a Comment