Friday, February 05, 2016

KAMBI YA UPINZANI YATANGAZA MAWAZIRI WAKE

Na Raymomd Mushumbusi-MAELEZO
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe Mbunge wa Hai (CHADEMA) ametangaza rasmi Baraza la Mawaziri vivuli litakalosaidiana na Serikali katika kuendesha shughuli za kimaendeleo.

Akitangaza Mawaziri hao vivuli kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani amesema anawaomba Mawaziri wa Wizara husika kuwapa ushirikiano wale wote walioteuliwa kuwa Mawaziri vivuli katika Kambi ya Upinzani ili kupeleka mbele gurudumu la maendeleo nchini.

Waliotangazwa Katika Orodha hiyo ni Pamoja na Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora Jaffar Michael, Manaibu wake ni Joseph Nkundi na Ruth Mollel, Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Ali Saleh Abdalla na Naibu wake ni Pauline Gekul, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu Esther Bulaya na Manaibu ni Yusuph Makame na Maftah Abdalla, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ina mawziri wawili ambao ni Magdalena Sakaaya na Emmaculate Swari Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Inj. James Mbatia na Naibu Waziri Willy Kombucha.


Aidha ameendelea kuwataja Mawaziri wengine kuwa ni Waziri ya Fedha na Mipango Halima Mdee na Naibu Waziri ni David Silinde, Waziri ya Nishati na Madini
John Mnyika na Naibu Waziri ni John Heche, Waziri ya Katiba na Sheria Tundu Lissu na Naibu Waziri Abdalla Mtolela, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Peter Msigwa na Naibu Waziri Riziki Shaghal, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Juma Omari na Naibu Waziri Mwita Waitara, Waziri ya Mambo ya Ndani Godbless Lema na Naibu Waziri Masoud Abdalla, Waziri ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilfred Lwakatare na
Naibu Waziri Salum Mgoso.

Wengine walioteuliwa katika Baraza kivuli ni Waziri wa Maliasili na Utalii Esther Matiko na Naibu Waziri– Cecilia Pareso, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Anthony Komu na Naibu Waziri Cecil Mwambe, Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi Suzan Lyimo Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto– Dkt. Godwin Mollel na Naibu Waziri Zubeda Sakul, Waziri wa Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo Joseph Mbilinyi na Naibu Waziri – Devotha Minja na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Hamidu Hassan na Naibu Waziri Peter Lijualikali.

No comments:

Post a Comment