Thursday, January 09, 2014

MAZITO YAZIDI KUIBUKA : SAMAKI AZIDI KUMTESA MTOTO, SOMA HAPA


Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bunda, Mika Nyange, ameagiza askari wake kufanyia uchunguzi taarifa za tukio la samaki aina ya sato kuruka na kuingia sehemu za siri na kisha kukimbilia tumboni mwa mtoto wa kike wenye umri wa miaka 12 (jina tunalo).


Tukio hilo linadaiwa kutokea Januari Mosi, mwaka huu wakati mtoto huyo akichota maji katika Ziwa Victoria ili aweze kumwagilia bustani. 
Akiwa amechuchumaa ndipo samaki huyo anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa inchi nne aliruka kutoka majini na kuingia sehemu zake za siri na kukimbilia tumboni.

SOMA ZAIDI...

Baba mdogo wa mtoto huyo, Lenatus Mtani, alidai baada ya kumfikisha Hospitali ya Wilaya Ukerewe, alipimwa lakini samaki huyo hakuonekana tumboni. 
"Hospitali baada ya kumpima walisema hawaoni kitu, lakini anapoenda kujisaidia haja ndogo mkia wa samaki unaonekana," alisema Mtani. 


Alisema wameamua kumrudisha mtoto huyo kwa waganga wa kienyeji ambapo hali inazidi kuwa mbaya kwani ameanza kutoa harufu mbaya sehemu za siri. 
Kuonekana kwa mkia wa samaki huyo kumethibitishwa na bibi yake, Imaculate Mtani (64) na Monica Faustine, ambao ndiyo wanaomhudumia.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu jana, OCD huyo wa Wilaya ya Bunda, alikiri kupata taarifa zisizo rasmi za tukio hilo kutoka kwa bwana mmoja ambaye hakumtaja jina. 


"Ndiyo nimepata taarifa zisizo rasmi za tukio hilo na nimeagiza askari wangu walifuatilie," alisema Nyange na kuongeza kwamba amepata taarifa kuwa mtoto huyo alipelekwa Hospitali ya Wilaya Ukerewe, lakini hawakupata msaada mzuri hivyo ikabidi wampeleke kwa waganga wa kienyeji. 


Aliongeza kuwa; "Nimeagiza askari wawafuate ndugu zake ili wampeleke hospitali kubwa." Pia alisema ameagiza Diwani wa Kata ya Napindi, Elias Magoti, kushirikiana na Polisi ili kufuatilia tukio hilo. 


Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Dkt. Hassan Mataka, alipoulizwa kama anafahamu tukio hilo, alisema halifahamu na kwamba kama kukitokea matukio ya ajabu huwa wanatoa taarifa. 
"Nimempigia Mganga Mfawidhi yeye ameniambia tukio hilo wamelisikia, lakini watu hao hawajafika hospitalini hapo," alisema Dkt.Mataka. Akizungumza na gazeti hili jana.


No comments:

Post a Comment